October 02, 2022

AT KUJAZA NAFASI ZILIZOWAZI NOV. 27

Katibu Mkuu wa AT, Wakili Jackson Ndaweka (Katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jana. Kushoto ni Mwenyekiti Kamati ya Ufundi  Michael Washa na Kulia ni Msemaji AT Lwiza John.



NA TULLO CHAMBO

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (AT), linatarajiwa kuziba nafasi za uongozi zailizo wazi Novemba 27 jijini Tanga.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa AT, Wakili Jackson Ndaweka,  alisema kikao cha Kamati Tendaji kilichofanyika jijini Dar Ess Salaam Oktoba Mosi chini ya Rais wa AT, Silas Isangi, kilijadili mambo mbalimbali ikiwamo kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wahusika waliojiuzulu kutokana na sababu mbalimbali mara baada ya uchaguzi wa Januari 2021.


Wakili Ndaweka, alisema wamepanga Novemba 25 na 26 kufanyika mashindano ya Taifa kabla ya Mkutano Mkuu na Uchaguzi huo Novemba 27.


"Katika kufanikisha uchaguzi huo, Kamati Tendaji iliteua Kamati ya Uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya AT, ikiwa na wajumbe sita ambao watasimamia jukumu hilo," alisema Wakili Ndaweka na kuongeza.


Kamati hiyo iitaundwa na Wakili Msomi Menrad D'souza ambaye atakuwa Mwenyekiti, Benjamin Karume Makamu Mwenyekiti huku wajumbe ni Morris Okinda, Dk. Hamad Ndee na Mwinga Mwanjala.


Aidha, Wakili Ndaweka, alisema Kamati Tendaji imemteua Lwiza John kuwa Msemaji mpya wa shirikisho hilo.


Nafasi ambazo ziko wazi na zinazotarajiwa kuzibwa ni Makamu wa Rais iliyokuwa ikishikiliwa na John Bayo na Mjumbe Kamati Tendaji Kanda ya Pwani Robert Kalyahe.


Kwa upande wake, Msemaji mpya wa AT, Lwiza John, aliomba waandishi wa habari kumpa ushirikiano katika kuujenga mchezo wa riadha na kwamba wasisite kuwasiliana naye pale wanapoona kuna mkanganyiko katika masuala mbalimbali yanayouhusu mchezo huo na atatoa ushirikiano wa kutosha.
 

Pia Kamati Tendaji ilijadili kusimamishwa kwa Mwenyekiti Kamisheni ya Wachezaji, Benjamin Michael, na kubaini kuna upungufu ulifanyika hivyo kumrejesha madarakani na Andrew Robbi aliyekuwa akikaimu atabaki kwenye nafasi yake ya Katibu.

No comments:

Post a Comment

Pages