October 04, 2022

Marafiki Festival siku nne Dar, Bagamoyo


 


MSIMU wa tatu wa Tamasha kubwa la Marafiki Music Festival umewadia ambapo kivumbi kizito cha burudani kinatazamiwa kuanza kutimka Alhamisi hii ndani ya Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam kwa mtonyo mdogo wa buku 15 tu.

Bosi wa Kampuni ya Asedeva ambao ndio waandaaji, Isack Abeneko, amesema bendi 20 pamoja na zaidi ya wasanii 128 kutoka mataifa mbalimbali Afrika, wakiwamo Man Fongo na Balaa MC kwa hapa nchini, wanatarajiwa kupamba shughuli hiyo.


"Tamasha la mwaka huu litakuwa ni la siku nne ambapo kuanzia Oktoba 6 hadi 8, litarindima hapa Dar es Salaam kabla ya Oktoba 9 kufunga dimba kwenye ukumbi wa Firefly, Bagamoyo, Pwani," amesema Abeneko na kuongeza:

"Viingilio kwenye shughuli hiyo vitakuwa ni sh 15,000 kwa watu wazima na 5,000 kwa wanafunzi watakaokuwa na vitambulisho vya shule, lakini pia tiketi za awali tayari zimeshaanza kuuzwa kwa bei ya sh 20,000 kwa shoo zote nne na 10,000 kwa tukio moja."

No comments:

Post a Comment

Pages