Na Victor Masangu, Pwani
Serikali
imesema kwamba kwa sasa hali ya kiwango cha uzalishaji wa maji katika
mto Ruvu kimepungua kwa asilimia 64 kutokana na kuwepo kwa changamoto
kubwa ukosefu wa mvua za vuli uliosabishwa na madaliko ya tabia ya nchi
na kupelekea kuwepo kwa ukame.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makala wakati wa
ziara ya bodi ya wakurugenzi wa Dawasa , pamoja Kamati ya ulinzi na
usalama ya Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea hali halisi ya kupungua
kwa kiwango cha maji.
Aidha
mkuu huyo akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa ya Pwani na Morogoro
amesema kwamba jitihada za serikali katika kuhakikisha maji yaliyopo
yanawafikia wananchi japo kwa mgao hadi hapo mvua zitakaponyesha.
Makala
alisema kwamba hali hiyo ya kupungua kwa kiwango maji katika mto ruvu
kumesababishwa na kukosekana kwa mvua za vuli hivyo kwa sasa
kutalazimika kuwa na mgao katika maeneo mbali mbali.
"Tumejionea
kushuka kwa kina na uzalishaji katika mitambo ya ruvu juu pamoja na
ruvu chini na kwa hali hii ni lazima tuchukue tahadhari na wananchi
wahakikishe kwamba wanatunza maji kwani yatakuwa ya mgao,"alisema
Makala.
Pia
Mkuu huyo ya Mkoa alibainisha kuwa kasi ya uwezo wa uzalishaji wa maji
umeshuka kutoka Lita Milioni 466 mpaka kufikia lita zipatazo Milioni
300 hivyo kiwango cha maji kimeoungua.
"Ndugu
zangu wananchi wa Mkoa wa Pwani pamoja na Dar es Salaam kumuomba Mungu
ili mvua ziweze kunyesha na kutumia vizuri kiasi cha maji yaliyopo ili
kuondokana na changamoto ya upatikanaji huo wa maji,"alibainisha Makala
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema tatizo la mgao wa maji katika jijini la Dar es
Salaam kwa Sasa ni matokeo ya kiangazi kilichosababishwa na kukosekana
kwa mvua za vuli jambo lililopelekea kushuka kwa kina Cha maji kwenye
vyanzo vya Maji Ruvu juu na ruvu chini.
Aidha
aliongeza Kamati za Ulinzi na usalama Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na
Morogoro zilishatekeleza wajibu katika kudhibiti uchepushaji wa maji
hivyo uhaba wa maji hauhusiani na uzembe wa mamlaka husika.

No comments:
Post a Comment