Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipokea maua kutoka kwa watoto Neviah Mwamlima (kushoto) na Bradley Massawe wakati walipowasili kwenye hoteli ya Lotte iliyopo Seoul nchini Korea ya Kusini, Oktoba 24, 2022 kuanza ziara ya kikazi nchini humo. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Togolani Mavura. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim. Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakisalimiana na baadhi ya watanzania waishio nchini Korea ya Kusini waakati walipowasili kwenye hoteli ya Lotte iliyopo Seoul nchini humo Oktoba 24, 2022 kwa ziara ya kikazi . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Korea
ya Kusini, Mhe. Togolani Mavura wakati alipowasili kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Incheon nchini Korea ya Kusini Oktoba 24, 2022
kwa ziara ya kikazi nchini humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa leo (Jumatatu, Oktoba 24, 2022) amewasili Seoul,
Jamhuri ya Korea Kusini kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Mheshimiwa
Majaliwa alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Togolani Mavura
pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi katika nchi hiyo.
Kesho
(Jumanne, Oktoba 25, 2022) Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea kkampuni
ya kutengeneza mabehewa na injini za treni cha SRT kilichopo katika mji
wa viwanda wa Mungyeong pamoja na kituo cha ubunifu kilichopo Pangyo.
Aidha,
akiwa Korea Kusini, Waziri Mkuu anatarajiwa kushiriki kongamano la
biashara na kukutana na wamiliki wa makampuni makubwa na wenye viwanda.
Vilevile, atakutana na Watanzania waishio Korea Kusini.




No comments:
Post a Comment