October 05, 2022

ZAKA ZAKAZI AFUATA NYAYO ZA MANARA


WAKATI Bado sakata la aliyekuwa Ofisa mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara likiwa bado linafukuta tangu alipopigwa nyundo wa miaka miwili ya kutojihusisha soka na faini ya million 20 kabla ya kupunguzwa.

Ofisa Habari wa Azam FC Thabiti Zakaria amekutana na rugu la Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara TPLB kwa kufungiwa miezi mitatu na faini juu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi inaeleza kuwa.

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Oktoba 4, 2022 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;
 

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabiti Zakaria amefungiwa kwa kipindi cha miezi mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kushutumu waamuzi wa mchezo tajwa hapo juu kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Thabiti alitenda kosa hilo huku akifahamu kuwa klabu yake ilikuwa imeshatumia njia sahihi ya kikanuni kwa kuiandikia barua Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuhusu malalamiko yao kwa Waamuzi.
 
Kanuni ya 39:(8 & 10) ya Ligi Kuu kuhusu Waamuzi na Kanuni ya
46:(3 & 10) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Viongozi zinasisitiza
Klabu kutumia njia sahihi kuwasilisha malalamiko yao kwa TPLB/TFF na kuwataka viongozi kuepuka kulalamika ama kushutumu waamuzi kupitia vyombo vya habari na mahali pengine popote.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 46:10 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Viongozi.
 
Hata hivyo mwamuzi wa kati wa mchezo tajwa hapo juu, Hans Mabena kutoka mkoani Tanga amepelekwa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria 17 za mpira wa miguu jambo lililosababisha ashindwe kumudu mchezo huo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Septemba 30, 2022.

Katika hatua nyingine Klabu ya Namungo imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la mashabiki kuingia eneo la kiufundi la mchezo mara baada ya mchezo tajwa hapo juu kumalizika.

Tukio hilo lilifanyika wakati watangazaji wa Azam TV (mdhamini mwenye haki za matangazo ya Televisheni) wakiendelea kufanya mahojiano na makocha.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
 
Kwingineko Mechi Namba 43: Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC  
Timu ya Dodoma Jiji imetozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuchelewa kutoka kwenye chumba cha kuvalia jambo lililosababisha mchezo tajwa hapo juu kuchelewa kuanza kwa dakika moja (1) na sekunde 30.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 17:(33 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
 

No comments:

Post a Comment

Pages