Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga (kushoto), akiteta jambo na wakili wake Edson Kilatu, baada ya kutoa ushahidi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam katika kesi iliyofunguliwa na wabunge wa Chadema waliovuliwa uanachama. (PICHA NA FRANCIS DANDE).
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Viti maalum kupitia Chadema, Hawa Mwaifunga amedai mahakamani kwamba nafasi pekee waliyopewa na Baraza Kuu la Chama hicho ni kuomba msamaha.
Mwaifunga
alidai hayo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakati
akijibu maswali ya wakili wa Chadema Peter Kibatala dhidi ya kesi
iliyofunguliwa na kina Halima Mdee kupinga kuvuliwa uawanachama wa chama
hicho.
Alidai mbele ya
Jaji Cyprian Mkeha, kuwa yeye na wenzake 18 waliitwa kuhudhuria kikao
cha Baraza Kuu la Chadema Mei 11 mwaka 2022 ambapo katika kikao hicho
walitakiwa kuthibitisha rufaa zao.
Mbunge
huyo alidai nafasi nyingine waliyopewa ni kuomba msamaha kabla wajumbe
wa baraza hilo kupiga kura na hafikia uamuzi wa kutangaza kuwavua
uanachama wao.
"Uamuzi wa baraza hilo ulitokana na utaratibu wa kupiga kura kila kanda, wajumbe 23 wa Kamati Kuu ya Chadema wakipiga kura hizo peke yao.
"Idadi
ya kura zilizopigwa na wajumbe hao ni 423 ambapo 413 walikubaliana na
uamuzi wa kutuvua uanachama, watano walikataa uamuzi na watano hawakuwa
na upande,"alidai.
"Katika
kiapo changu sikueleza kama Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu
John Mnyika walikuwepo katika kikao cha Baraza Kuu kilichowafukuza
uanachama kwasababu Katiba ya chama hicho inaeleza wanaoongoza vikao vya
kufanya maamuzi, "alidai mbunge huyo.
Mdee na wenzake 18 wanapinga kuvuliwa ubunge na Baraza Kuu la Chadema.

No comments:
Post a Comment