Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa tisa wa dawa za kulevya.
Mwandishi Wetu
KOCHA
wa Makipa wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam Muharami Sultan
(40) mkazi wa Kigamboni na wenzake wanane wanashikiliwa na Mamla ya Dawa
za Kilevya nchini, kwa kukutwa na kilo 34.89 za herion.
Akizungumza
na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kamishna
Generali Gerald Kusaya wa Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za
Kulevya alisema mamlaka yake imefanikiwa kuwakamata watuhumia hao mahali
tofauti nchini.
Alisema
mbali na Sultani wengine ni, mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sports
Academy, Kambi Seif maarufu kama Alhaji Kambi (40) mkazi wa
Oysterbay, Fundi Seremala, Said Matwiko (41) mkazi wa Kivule na
mkulima, Maulid Mzungu maarufu kama Mbonde (54) mkazi wa Kamegele
Kisemvule.
Wengine ni,
mfanyabiasha John John maarufu kama Chipanda (40) mkazi wa Magore
Kitunda, Rajabu Dhahabu (32) mkazi wa Tabata Segerea, mkulima Seleman
Matola Said (24) ambaye ni mtoto wa dada yake Alhaji Kambi, Hussein Pazi
(41) mkazi wa Kibugumo Kigamboni na Ramadhani Chalamila (27) mkazi wa
Mzinga Kongowe.
Alisema bado upelelezi unaendelea kuwasaka watuhumia wengine na kwamba wakati wowote watuhumiwa watafikisha mahakamani.
Mbali
na watuhumiwa tisa, mamlaka inawashikilia watuhumiwa wengine wawili kwa
kukutwa na biskuti 50 zilizotengenezwa na Dawa za Kulevya aina ya
bangi.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni, Abnasir Kombo mkazi wa Kaloleni Arusha akiwa na biskuti 50 zilizotengenezwa na bangi.
Mwingine ni,mtengenezaji wa biskuti Hassan Ismail (25) mkazi wa Arusha.
"Serikali
haijalala bado tunaendelea na msako nchi nzima kwa wakae wakijua
magereza yako wazi na wanaotarajia kutajirika na Dawa za Kulevya
wasijisumbue tutawadaka"alisema Kamishna Kusaya.
Alisema watanzania wote washirikiane na mamlaka kufichua wanaojihusisha na Dawa za Kulevya nchini kuokoa maisha ya watanzania.


No comments:
Post a Comment