Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Sagini, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa Sera ya Ubia ya Shirika hilo utakaofanyika Novemba 16, mwaka huu. PICHA: MTANDAO.
SHIRIKA
la Nyumba la Taifa (NHC), limesema kwamba takribani wadau 1,000
wanaotarajia kukutana nchini, Novemba 16, mwaka huu, lengo kwenye
uzinduzi wa Sera ya Ubia na kujadili fursa za ubia hususan ujenzi wa
majengo.
Kati ya
washiriki hao taasisi za kimataifa ni 10, balozi zaidi ya 20, kamati
mbalimbali za bunge pamoja na taasisi za fedha na wawekezaji wa ndani na
nje ya nchi.
Meneja
Habari na Uhusiano wa shirika hilo, Muungano Saguya, aliyasema hayo
mwishoni mwa wiki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, akisema matokeo ya uzinduzi huo ni baada ya kutangazwa kwa Sera
Ubia iliyoboreshwa.
Alisema
mkutano huo ambao utafanyika jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi
akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kwamba mwitikio mkubwa
upo kutoka makampuni binafsi ya ndani na nje ya nchi.
“Washiriki
katika uzinduzi huu ni taasisi za Serikali, vyama na bodi za kitaaluma,
pamoja na wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi ambao tayari
wamethibitisha kushiriki.
“Katika
uzinduzi pia zaidi ya Balozi 20 na Taasisi za Kimataifa 10 zitashiriki,
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Wenyeviti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Uwekezaji na
Mitaji ya Umma (PIC), Mawaziri, Mhimili wa Mahakama na Taasisi za Fedha.
“Kutokana
na hali hiyo, Shirika limeona ni vema kuchambua na kuainisha zaidi
maeneo ya kutosha ya kukidhi shauku hiyo ya kujenga nchi yetu, hapo
awali tulitenga maeneo 60 tu yenye viwanja au majengo yanayohitaji
kuendelezwa. Kwa msukumo uliopo sasa, tumeamua kuongeza maeneo zaidi ili
yaendelezwe,” alisema Saguya.
Alisema,
Shirika hilo linatayarisha vitabu viwili vitakavyoelezea sera hiyo na
maeneo ya uwekezaji ya NHC yaliyopo, ikiwamo maeneo yenye majengo
chakavu.
“Kuzinduliwa kwa
Sera ya Ubia kunaenda kufungua milango ya uwekezaji kwenye sekta ya
nyumba na kwamba Shirika linaunga mkono, maono na maelekezo ya Rais
Samia Hassan ya kuvutia wawekezaji nchini kwa kuruhusu sekta binafsi
ambayo ni injini ya kuleta na kujenga uchumi wa Taifa letu,” alisema
Saguya.


No comments:
Post a Comment