November 06, 2022

PSSSF yahadharisha tozo kuchelewesha michango


 
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Kanda ya Temeke, Rajabu Kinande, akitoa mada katika Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Da es Salaam (DCPC), uliofanyika leo Novemba 6, 2022 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji DCPC. (NA MPIGA PICHA WETU).

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo, akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Da es Salaam (DCPC).

 


 
Meneja Mawasiliano swa TCRA, Semu Mwakanjala, akitoa mada katika Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Da es Salaam (DCPC), uliofanyika leo Novemba 6, 2022 jijini Dar es Salaam. 

Baaadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Da es Salaam (DCPC).

  

Na Mwandishi Wetu

 

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetanabaisha kuwa kitendo cha waajiri kuchelewesha  michango ya watumishi kinasababisha  tozo ya ucheleweshaji wakati wa kulipa mafao kwa wanachama.

 

Akizungumza  leo Novemba 6, 2022 jijini Dar es Salaam, wakati wa Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC), Meneja wa PSSSF Temeke, Rajabu Kinande amesema kitendo cha mwajiri kuchelewesha mchango huo kunaathiri mafao ya mwanachama.


"Ili kupunguza malalamiko ni vyema waajiri kutimiza wajibu wao kisheria wa kulipa michango ya watumishi wake ndani ya mwezi mmoja baada ya mwisho wa mwezi husika" amesema Kinande.

 

 Kinande amesema utaratibu wa kufanya malipo upo kiteknolojia ambapo kumbukumbu za malipo zitahifadhiwa.


"Kwa sasa mwajiri ana uwezo wa kutengeneza namba za kumbukumbu ya malipo itakayomuwezesha kulipa michango na kupata risiti kupitia mtandao," alieleza. 

 

Wakati huo huo Kinande amesema wastaafu wengi wanachelewa kupata mafao yao kutokana na kuchelewesha taarifa zao za kustaafu kabla ya miezi sita.

Aidha, umesema kuwa hakuna watumishi wanaowafanyia mpango wastaafu wengine kupata mafao mapema badala yake uwahishaji wa taarifa zao ndio unawasaidia kupata stahiki zao haraka.


Amesema baada ya kupata taarifa hiyo, mtumishi anatakiwa kuanza kufuatilia mafao yake kwa kupeleka taarifa zote muhimu katika ofisi hizo ili zianze kufanyiwa kazi ikiwemo kufuatilia kama waajiri wamechangia miezi yote kama inavyotakiwa na sheria.


Alisema kila mwaka mfuko huo hufanya uhakiki wa wastaafu na wategemezi wanaopata pensheni kwa lengo la kusafisha daftari la wastaafu na kuhakikisha pensheni inalipwa kwa walengwa na si vinginevyo.

No comments:

Post a Comment

Pages