Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi pamoja na Wananchi waliohudhuria kwenye Kongamano la Kitaifa kuhusu Nishati Safi ya Kupikia katika Ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC).
Rais Samia akiwa na viongozi.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameelekeza
kuundwa kwa Kikosi Kazi kitakacho shughulikia Nishati Safi ya kupikia
nchini lengo likiwa kulitoa Taifa kwenye matumizi ya nishati zisizofaa.
Kauli
hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la la
Kitaifa kuhusu Nishati Safi ya Kupikia katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere(JNICC).
Amesema
kuwa kikosi kazi hicho hakitakuwa cha Serikali pekee, bali kitahusisha
pia sekta binafsi na wadau wa maendeleo na kitakuwa na kazi ya kuchambua
sera za Serikali pamoja na mapendekezo ya wadau.
Amebainisha
kuwa kikosi kazi hicho kitaongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa
ngazi ya mawaziri na uratibu zote zitafanyika chini ya Wizara ya
Nishati.
"Kikosi
kazi hicho kitakuja na mpango mkakati ambao utaiongoza Serikali, sekta
binafsi na wadau wa maendeleo kutafuta suluhu ya nishati safi na
endelevu ya kupikia" Alisema rais Samia.
Amesisitiza
kuwa kwa mujibu takwimu zilizopo kaya zinazopikia kwa kutumia mitungi
ya gesi ni asilimia 5, umeme asilimia 3 na nishati nyingine safi
asilimia 2.2.
Hivyo
bado kuna kazi ya kubwa ya kuhamasisha matumizi ya nishati iliyo safi
na salama na pia tunapaswa kuwa na mkakati madhubuti wa kisera na
kibajeti pamoja na kuweka mazingira wezeshi katika kutatua changamoto za
upatikanaji wa nishati safi.
“Serikali
peke yetu hatuwezi tunapaswa kwenda sambamba na sekta binafsi,
nashukuru baadhi yao wameanza kujitokeza kushirikiana nao sambamba
lakini si kisera kutokana kuwa ni fursa ya biashara hivyo kuna haja ya
kuwa na sera inayoshughulikia suala hili,” Amesema Rais Samia
Katika
hatua nyingine,Rais Samia amesema kuanzia bajeti ijayo, Serikali
itatenga fedha za kutosha zitakazoanzisha mfuko wa nishati safi ya
kupikia lengo ni kwenda kumtua mama mzigo wa kuni kichwani.
Awali
Profesa, Anna Tibaijuka ameishauri Serikali kuweka utaratibu mzuri wa
kibiashara kwa wauzaji wa nishati ya gesi ili waweze kuyafikia maeneo
mengi hasa ya vijijini.
Amesema
kuwa sehemu kubwa ya wananchi wa Vijijini wamekuwa wakikumbana na adha
ya utafutaji wa kuni kwa ajili ya kupikia kitu ambacho kimekuwa
kikiwapotezea muda mwingi wa kufanya shughuli za kuinua vipato vyao na
hivyo kushindwa kumudu gharama za maisha.
“Mimi
mwenyewe ni muhanga wa watu walikuwa wakikumbana na adha ya utafutaji
kuni hivyo naelewa fika suala hili kama kweli mjadala huu unalenga
kuleta unafuu ni wazi kwamba tunahitajika kuchukua hatua rafiki kwa
kuwashirikisha Wafanyabiashara wa gesi,”amefafanua Tibaijuka.
Hata
hivyo ameshauri Serikali pia kuangalia gharama za upandaji wa vitu
mbalimbali na kuziweka katika hali rafiki kwa kila nyanja ili kuepuka
kuleta nafuu ya jambo moja huku mengine yakiendelea kuwakandamiza
wananchi.
Kwa
upande wake, Waziri wa Nishati, January, amesema kongamano hilo
linalenga kuwaokoa maelefu ya Watanzania ambao wamekuwa wakiathirika
kutokana na kutumia nishati inayotokana na kuni, mkaa na mabaki ya mazao
na vinyesi vya wanyama.
Takwimu
zinaonyesha kuwa, zaidi ya watu 30,000 wanapoteza maisha kila mwaka
kutokana na kutumia nishati ya kuni na mkaa ambayo, kiafya sio salama
lakini kutokana na changamoto mbalimbali imewalazimu kutumia.
..jpg)


No comments:
Post a Comment