Na Mwandishi Wetu
Haikuwa bahati kwa wawakilishi wa Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Simba Queens kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa Soka la Wanawake Afrika CAF WCL.
Ndio kauli inayoweza kuelezea kiwango bora walichokionyesha katika mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya Mamelod Soundwns licha ya kupoteza bao (1-0).
Simba walikuwa bora sana katika eneo la ulinzi na kiungo kiasi cha kuzima ubora wa Mamelod kucheza mpira wao.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Kocha Mkuu wa Simba Queens Charles Lukula amesema haikuwa bahati kwao kwani walicheza vizuri kuliko wapinzani wao.
"Kwangu mimi tumecheza vizur, tumekosa bahati ya kutumia nafasi zetu, kipindi cha pili pia tulipata nafasi hatukuweza kuzitumia labda ni bahati tumekosa ila nawapongeza wachezaji wangu wamecheza vizuri."
"Maamuzi hayakuwa sawa, tumeadhibiwa kwa makosa ambayo wenzetu walikuwa wanapewa onyo tu, hata goli tulilofungwa tulitoka kuchezewa madhambi mwamuzi akapeta tukafungwa, kiufupi maamuzi hayakuwa sawa" Lukula ameongeza kuwa
"Nadhani tunahitaji kuongeza mshambuliaji mwingine Ili tusiwe tunamtegemea Oppah pekeake, hii itatusaidia na kuisaidia timu."
Kwa matokeo hayo Simba Queens wanasubiri kucheza mchezo wa kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Beyesla Queens ya Nigeria.

No comments:
Post a Comment