HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 12, 2022

SIMBA SC NA KITANZI CHA UBINGWA NPL


WAKATI Klabu ya Simba ikitarajiwa kurejea kesho kwenye Dimba la Benjamin Mkapa kuwakabili Ihefu FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NPL, mwenendo wao wa kuusaka ubingwa unazidi kutia mashaka.

Simba wametoka kupata sare dhidi ya Singida Big Stars ya bao (1-1) mtanange uliounguruma siku mbili zilziopita Mkoani Singida.

Sare hiyo inakuwa ya tatu msimu huu katika michezo tisa waliocheza huku wakiwa wameshapoteza mchezo mmoja.

Bahati mbaya kwa Simba wamedondosha pointi kwa timu ambazo wako pamoja katika mbio za ubingwa, Sare ya kwanza dhidi ya KMC FC ya mabao 2-2, dhidi ya Yanga SC 1-1, dhidi ya Singida BS 1-1 huku wakipoteza bao 1-0 dhidi ya Azam FC.

Kwa muktadha huo Simba wameangusha pointi tisa kati ya 27 za michezo tisa waliyoshuka dimbani na sasa wana pointi 18 licha ya kuwa ndo timu iliyofunga mabao mengi hadi sasa 18.

Katika hizo pointi tisa walizodondosha saba wameziangusha dhidi ya wapinzani wake ambao wako sambamba kwenye mbio za ubingwa.

Wanetoka sare na Yanga kinara wa Ligi pointi 20 michezo nane, wamepoteza kwa Azam FC bao 1-0 ambao wako nafasi ya pili pointi 20 michezo 10 na sare dhidi ya Singida BS, ambao wako nafasi ya nne pointi 18 michezo 10.

Kwa mwenendo huo Simba inaonyesha kupitia wakati mgumu sana kuishi kwenye ndoto zao za kutaka kuurejesha ubingwa waliopokwa na watani zao msimu uliopita.

Swali ni je Simba kwa mwenendo huo wanajiondoa kwenye mbio za ubingwa ama bado wanakazi ya kufanya?

No comments:

Post a Comment

Pages