November 02, 2022

WAIMBAJI MAARUFU NYIMBO ZA INJILI KUSHIRIKI TAMASHA LA KUMUOMBEA RAIS SAMIA MWANZA

 

Mratibu wa Tamasha la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan, Emmanuel Mabisa, akizungumza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 2, 2022 kuhusu uzinduzi wa Tamasha kubwa la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan litakalofanyika Novemba 6 jijini Mwanza. Tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion.

Mwimbaji mahiri wanyimbo za injili Rose Mhando, akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 2, 2022 kuhusu uzinduzi wa Tamasha kubwa la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan litakalofanyika Novemba 6 jijini Mwanza. Tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion.


Na Francis Dande

 

WAKAZI wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa Tamasha kubwa la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan litakalofanyika Novemba 6, 2022.

 

Mratibu wa Tamasha hilo ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mabisa amesema kuwa uzinduzi utafanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku viingilio vikiwa shilingi 2000 kwa watu wazima na watoto 1000 na milango itakuwa wazi kuanzia asubuhi ili kutoa fursa kwa watu wengi kushuhudia tamasha hilo.

 

“Mimi pia nitakuwepo, nikiwa kama mtanzania na msanii wa nyimbo za injili na mdau wa sanaa nimeona niungane na wenzangu pamoja na Msama Promotion kwa ajili ya kumuombea Rais wetu”.`alisema Mabise.

 

Kwa upande wa wasanii wa nyimbo za injili Rose Mhando alisema kuwa walikuwa hawajawahi kupokea mirahaba lakini katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia wameweza kupokea pesa nyingi, “kwa mfano kama mimi na wenzangu tumepokea pesa nzuri tu, kwa hiyo mungu ambariki kwa kutoa fursa nyingi.

 

Mhando amewata wakazi wa Mwanza na mikoa jirani wasipitwe na tamasha hilo siku ya Jumapili Novemba 6, 2022 ni siku maalumu kabisa imetengwa kwa ajili ya kumuombea Rais Samia na kumkabidhi mikononi mwa Mungu ili aendelee kufanya kazi kubwa ya kuongoza nchi na taifa kwa ujumla, kumpa hongera kwa kazi kubwa aliyoifanya tangu alipoingia madarakani.


 

"Yamepita mambo mengi magumu katika taifa letu lakini amepambana, amefanya Royal Tour, amesababisha taifa limeingiza watalii wengi kwa nini tusifanye asante alisema". Rose Mhando.


 

Waimbaji mahiri wakataokuwepo katika kulipamba tamasha hilo ni pamoja na Christine Shusho, Rose Mhando na Zabron Singers na waimbaji wengine, 

 

Aidha waimbaji kutoka nchi jirani pia wamedhibitisha kushiriki katika uzinduzi huo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana.

No comments:

Post a Comment

Pages