November 01, 2022

YANGA HASIRA ZOTE KWA CLUB AFRICAIN


 

Na John Richard Marwa

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Nasriddine Nabi amesema hakuna wanachotaka zaidi ya kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC.

Amesema hayo kuelekea mchezo wa kwanza wa mtoano kusaka tiketi ya kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC dhidi ya Club Africain ya Tunisia hapo kesho kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.

"Maandalizi ya mechi ya kesho, tumejiandaa japo muda ni mchache, tulichokinya ni kuwafuatilia wapinzani wetu na kuwapa wachezaji nini wanaenda kufanya."

"Tumekosa muda wa maandalizi kwa kucheza mechi karibu karibu, TFF tuliwaomba mechi ya Geita waiondoe kwenye ratiba lakini haikuwa hivyo licha ya kuwa tunaiwakilisha nchi."amesema Nabi na kubainisha kuwa.

"Tumepata majeruhi wachezaji wawili ambao kesho hawatakuwepo. Lakini wana morali ya juu na wanahitaji kufanya vizuri na kuwafurahisha mashabiki wao."

"Kuna mechi mbili za kucheza na tunaamini kuwa tutafanya vizuri Ili kutinga hatua inayofuata." amesema Nabi.

Nabi ameeleza kuwa "Club Africain ni timu bora na nzuri hivyo wachezaji wanalitambua hilo na wameniahidi hilo kuwa watafanya vizuri."

Mpira ni mchezo ambao sio ndoto lakini ni uhalisia wa matendo kwa timu zote mbili, hivyo hakuna sababu ya kuwa na presha."ameongeza Nabi.

"Siwezi kusema wachezaji ambao ntaenda kuwakosa kwa sababu ntawapa nafasi wapinzani kuja na maswali kwetu hivyo tusubiri kesho tutajua maana yawezekana nikawakosa wachezaji muhimu na tegemeo hivyo siwezi kusema."

"Sio sababu ni timu ya nyumbani kwamba nikiwatoa ntafurahi ama wakinitoa ntahuzunika. Nilipo fika sihitaji kutafuta umaarufu wa mitandao ama vyombo vya habari. Kubwa nachohitaji zaidi ni kupata matokeo kwa ajili ya mashabiki wa Yanga SC." Kocha Nabi.

Kwa upande wa wachezaji Yusuph Athuman amesema, "
Kama wachezaji tuko tayari kwa ajili ya mapambano ya kusaka ushindi tuweze kutinga hatua ya makundi."

"Sisi  kama wachezaji tunafahamu umuhimu wa mchezo huu, malengo yetu yalikuwa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa lakini haijawa hivyo Sasa nguvu zote tunaelekeza kwenye michezo hii miwili." Yusuph Athuman.

No comments:

Post a Comment

Pages