Na Happiness Katabazi, Liwale
MBUNGE wa Jimbo la Liwale Zuberi Kuchauka amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa Jengo jipya la Utawala linalojengwa na halmashauri ya wilaya ya Liwale Mkoani Lindi.
Kuchauka ambaye alikuwa ameongozana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Liwale ,Milingo Kindamba jana katika ziara yake ya siku Moja ya kutembelea ujenzi wa Jengo Hilo la Utawala lilipo Liwale mjini ambalo litagharimu Sh Bilioni 3.8 alisema anaimani ujenzi huo utamalizika Kwa wakati.
" Kwanza tunamshukuru Rais Samia Suluhu kutuletea kiasi hicho Cha fedha kwaajili ya Jengo hili la kisasa ...lakini pia napenda kuwatia moyo wote mnaoshiriki ktk ujenzi huu kwani kasi yenu ya ujenzi ni nzuri na tunaimani Jengo litakamilika Kwa wakati hasa ukizingatia tayari fedha zipo." Alisema Mbunge Kuchauka.
Mhandisi mshauri toka Bureau For Industrial Corporation ( BICO) ,Eliudi Meteine akisoma ripoti ya ujenzi wa jengo hilo alisema Jengo Hilo ni Jengo la ghorofa Moja linajengwa na halmashauri ya Liwale na lina mkataba wa miaka miwili na mkataba huo umeanza Oktoba 5 mwaka huu na utakamilika 0ktoba 4 mwaka 2023 na ujenzi ulianza Oktoba mwaka huu.
Meteine alisema Jengo Hilo lenye thamani ya Sh 3,862,204,972 Lina mkataba wa thamani ya Sh 644,923,000 Kwa ajiru ya ufundi wa Jengo Zima ambapo mpaka Sasa fundi ameshalipwa fedha za awali Sh 96,738,450 sawa na asilimia 15 ya thamani ya mkataba wa fundi.
CHANZO: Gazeti la Habari Leo Desemba 30, 2022
No comments:
Post a Comment