December 26, 2022

SIMBA SC NA MVUA YA MABAO DAMU DAMU

 



Na Mwandishi Wetu


Klabu ya Simba SC imefikisha mabao 40 katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL) baada ya kuwbugiza KMC FC mabao (1-3) mchezo wa raundi ya 18 ya msimu wa 2022/23.



Mchezo huo uliolindima Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza KMC walikuwa wenyeji wakiwaalika Simba jioni ya leo na kukubali kipigo hiko ikiwa ni mara ya kwanza msimu huu kuruhusu mabao zaidi ya mawili.


Mchezo ulikuwa wa wazi kwa pande zote huku ukianza kwa kasi ya kati kwa timu zote kutumia mipira mirefu kushambulia, ni kama mpango waliokuwa nao KMC kuwazuia Simba kulitumia eneo la kati kuuzuia ubora wa Chama kuathiri eneo lao.


Wakati KMC wakifiri hivyo Simba wlikuja na njia ya tofauti kwa kumuweka Chama chini kama kiungo wa ulinzi huku Kanoute na Mzamiru Yassin wakiwa juu yake na kumfanya aanze kuyapanga mashambulizi kutokea chini hapa vungo wa ulinzi wa KMC waliingia kwenye mtengo Majogoro,  Nzigamasabho na Awesu Awesu kulazimika kupanda juu ili kudhibiti pasi za Chama na hapo hapo Chama akapiga pasi ya ku chopi kwa Shomary Kapombe alitoa pasi ya bao kwa John Bocco.


Kipindi cha pili KMC walikuja na kushambulia lango la Simba na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Sadala Lipangile, bao hilo liliwatoa Simba mafichoni na kuanza kulisakama lango la KMC na kuwaza kufunga mabao mawili na mtanange kutamatika kwa mabao (1-3).


Kwa ushindi huo Simba wamefikisha pointi 40 nyuma ya vinara Yanga SC wenye pointi 46, huku wakiwaacha Azam FC nafasi ya tatu na pointi zao 36.


Simba ndo klabu pekee yenye mabao mengi hadi sasa wakicheza mechi 18 na kufunga mabao 40 huku wakiwa ndo timu iliyoruhusu idadi ndogo ya mabao 9.


Clatous Chota Chama Mwamba wa Lusaka amefikisha pasi za mabao 10 msimu huu huku akiwa amefunga mabao matatu na John Bocco akiendelea kuzifumania nyavu akifikisha mabao sita msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Pages