December 27, 2022

SIMU YA FEI TOTO 'BETRI LOW'

 Na Mwandishi Wetu


Siku chache zilizopita lililibuka sakata la kiungo nyota wa Klabu ya Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' kuvunja mkataba na waajiri wake kwa madai ya kusaka maslahi bora zaidi nje ya Yanga ambapo amekosa kuthaminika kutokana na mchango mkubwa anautoa klabuni hapo.



Kwa mujibu wa Barua ya Feisa kwa Yanga alivunja mkataba kwa kutumia moja ya vipengele vya mkataba wake ambavyo vinampa nafasi ya kufanya hivyo kwa kurejesha fedha za usajili na mishahara ya miezi mitatu na Feisal alifanya hivyo kwa kurejesha milioni 100 za usajili pamoja na million 12 mshahara wa miezi mitatu ikiwa kila mwezi ni million nne.


Baada hayo kuibuka taharuki imekuwa kubwa hasa inapotajwa kuwa anatimkia kwa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC, viongozi wa Yanga wamepagawa kutaka suluhu dhidi ya Feisal japo mambo yamekuwa magumu kwao.


Wakati Feisal akitia ngumu Yanga imesisitiza, Fei ni mali yao hadi Mei 30, 2024 mkataba huo utakapomalizika na tayari imezirejesha fedha zilizowekwa na kiungo huyo, huku wakiendelea kumbembelea asaini mkataba mpya na kumuahidi kumboreshea mshahara wake kutoka Sh 4 Milioni hadi 20 Milioni.


Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Feisal ameimbia Habari Mseto Blog, kwamba Uongozi wa Yanga umekuwa ukimtumia mmoja watu wenye ushawishi kumlainisha kiungo huyo na hajaweza kufua dafu na sasa vigogo kutoka serikalini wakishindana kumtwangia simu kwa nia ya kumtaka abadili mawazo, simu zinazopelekea chaji kukata.


"Kuna msululu wa simu za vigogo kadhaa kutoka Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar wanampigia simu kumsihi arejesha moyo wake Young Africans kumaliza sakata hilo lakini Feisal ameweka ngumu na kubakia na msimamo wake.


"Licha ya simu za viongozi hao kiserikali kushindana, Feisal na Moyo wake ameshafunga ukurasa kuhusu yeye na Wananchi na anachotaka ni kuanza maisha mapya nje ya mitaa ya Twiga na Jangwani" kimeeleza chanzo hicho na kuongeza kuwa.


“Simu zimekuwa nyingi kwenye simu ya Feisal kiasi cha simu kuisha chaji na simu nyingine akilazimika kuzikwepa na zingine zimekuwa na vitisho kwake huku zingine zikimtaka kurejea kwenye meza ya mazungumzo na waajiri wake.


"Ni kama Feisal hana tena hisia na Yanga, ni kama moyoni mwake ukurasa wake na Yanga umefungwa na sasa unahitaji maisha mapya, mapenzi mapya na mazingira tofauti." Kilieleza chanzo hicho.


“Feisal anadai ni uamuzi mgumu amechukua kwani anaamini kipaji chake ndio mkombozi wake maana hana taalum nyingine, lakini aliwaza mbali, hajasoma, na soka ndio kila kitu kwake, hivyo anatamani kipaji chake kiwe suluhu dhidi maisha yake ya sasa na baadae. 


Kiliongeza nyota huyo amewekwa chini ya ulinzi kuhakikisha usalama wake ili aweze kuutuliza akili yake kwa  kinachoendelea baada ya  kuvunja kandarasi hiyo na kutaka kuanza maisha mapya.

No comments:

Post a Comment

Pages