Bingwa wa mashindano ya Pool ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi, Abdallah Hussein akifurahia Medali ya Dhahabu, Pesa taslimu shilingi 250,000/= pamoja na tuzo maalumu ya mashindano hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Klabu ya Snipers Mwenge jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam, Tanzania
MCHEZAJI wa Pooltable kutoka Klabu ya Snipers yenye makazi yake Mwenge Mpakani jijini Dar es Salaaam, Abdallah Hussein ameibuka Bingwa kwenye Mashindano ya mchezo wa Pool katika kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi na hivyo kuzawadiwa Medali ya Dhahabu, Pesa taslimu Shilingi 250,000/= pamoja na tuzo maalumu ya mashindano hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Snipers Klabu Mwenge jijini Dar es Salaam.
Abdallah Husein ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Pooltable alipata ubingwa huo kwa kumfunga Jackson Steven 9 – 6 katika fainali ilifanyika katika Klabu ya Snipers Mwenge Mpakani iyojumuisha wachezaji 32 wa Jijiji la Dar es Salaam kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi.
Jackson Steven alikamata nafasi ya pili ambapo alizawadiwa Medali ya Dhahabu pamoja na Pesa taslimu Shilingi 100,000/=
Mshindi wa tatu katika Mashindano hayo ni Patrick Nyangusi ambaye alipata nafasi hiyo kwa kumfunga Charles Venance kwa penati ya 7 – 6 na hivyo kuzawadiwa Medali ya Dhahabu na Pesa taslimu Shilingi 40,000/=
Patrick Nyangusi pamoja na kukamata nafasi ya tatu pia alishinda nafasi ya uchezaji bora wa mashindano na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi 50,000/=
Katika mashindano hayo pia kulikuwa na nafasi ya mchezaji aliyeonyesha nizamu bora katika mashindano ya maadhimsho ya miaka 59 ya Mapinduzi ambayo ilikwenda kwa Khalid Kondo ambaye alizawadiwa pesa taslimu shilingi 50,000/=
Akizungumza mara baada ya zoezi la zawadi, Mkurugenzi wa Snipers Klubu aliwapongeza Wachezaji na Wadau wote waliojitokeza katika Mashindano hayo ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi na kuwaomba Wadau wote tuendelee kushikamana ili mchezo wetu ufike tunapopahitaji kwa pamoja.
Maakamba pia aliwapongeza wote waliofanikiwa kushinda na kuzawadiwa zawadi kwani safari ya ushindi wao haikuwa nyepesi ni dhahili walipambana sana.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Isach Togocho aliwapongeza Snipers Klabu kupitia Mkurugenzi wa Klabu hiyo, Willfred Makamba, kwa kuandaa na kufadhili mashindano hayo ya maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi kwani jambo hilo ni heshima kubwa kwa Chama cha Pool laakini pia kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanyika kwa Mashindano hayo.
Pili aliwapongeza wachezaji wote waliojitokeza kushiriki mashindano hayo pamoja na mashabiki pia waliojitokeza kushuhudia lakini Zaidi aliwapongeza wote waliofanikiwa kushinda na kupata zawadi na kuwaomba zawadi hizo zikawe chachu ya kuwafanya wajiandae vyema na mashindano mengine yajayo.
Aidha pia Togocho alitoa taarifa kuwa mwaka huu kutakuwa na uchaguzi ndani ya chama cha pool ambao utagusa ngazi ya Taifa tu hivyo wadau wote tujiandae na uchagguzi huo.
Togocho alimaliza kwatoa taarifa pia mwezi Octoba kutakuwa na Mashindano ya Pool ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Nchini Afrika Kusini.Hivyo wachezaji na Wadau tujiandae kisaikolojia wakati wowote timu ya Taifa itaitwa na kuingia Kambini kwani lazima tushiriki.
No comments:
Post a Comment