Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kampuni
ya JATU PLC imetangaza kuwa imerejesha shughuli za Makao yake Makuu
Jijini Dar es Salaam kutoka Wilayani Sumbawanga,Mkoani Rukwa
zilikoahamishiwa mnamo mwaka jana.
Hayo
yamesemwa Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo,
Mohamed Simbano alipokuwa Akizungumza na wanahabari jijini humo juu ya
ujio wa Mtaalamu wa Masuala ya Fedha, Miradi na Biashara kutoka Nchini
Uholanzi ambaye atakuwepo nchini kwa majuma mawili kusaidia kampuni hiyo
kutengeneza mpango kazi mpya wa biashara itakayoendana na dira na
maono ya kuanzishwa kwa JATU PLC.
Amesema
kuwa tangu kampuni hiyo ilipofanya mabadiliko ya uongozi mwezi Agosti
mwaka jana wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kuirejesha kampuni
hiyo ambayo ilipitia changamoto mbalimbali na tayari wamesharudisha
baadhi ya huduma za uzalishaji wa unga wa Dona na Sembe katika ofisi zao
ndogo zilizopo Kinyerezi Jijini hapa.
"Ndugu
wanahabari kwasasa tumewekeza nguvu kubwa zaidi shambani mwaka huu wa
2023 ili kuongeza mapato zaidi na spidi ya kupunguza madeni pia
tumerudisha ofisi zetu za makao makuu hapa jengo la PSSSF HOUSE" amesema
Simbano.
Akizungumzia
Kuhusu ujio wa mtaalamu huyo wa masuala ya fedha miradi na baishara
kutoka nchini Uholanzi, Simbano amesema kuwa mgeni huyo aliyeingia
nchini January 2 mwaka huu kwa ushirikiano wa taasisi ya PUM Netherlands
Senior Experts ataungana na wataalamu wa masuala ya fedha na mitaji
ambao ni Luzane Financing na Kampuni ya Ushauri wa Kibiashara ya
InterCapital kwa kushirikiana na SSS Capital zote kutoka Tanzania na
watafanya kazi ya kuandalia kampuni ya JATU PLC mpango kazi mpya wa
biashara, kushauri juu ya mabadiliko yanayoendelea.
Kazi
nyingine zitakazofanywa kwa ushirikiano wa makampuni hayo ni pamoja na
kushauri juu ya kukuza mtaji na kulipa madeni yote kwa kuketi chini na
wadai wote kuona namna ya kuendesha miradi iliyokuwepo kuisimamia kwa
weledi na ujuzi ili kuleta tija na hatimaye kumaliza kabisa changamoto
zilizojitokeza.
Amebainisha
kuwa kampuni hiyo itashirikisha wadau wengine wa ndani na nje ya nchi
ambao ni wanahisa, wakulima, washauri, taasisi za kiserikali na wahisani
ili kuweza kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya uongozi wa JATU PLC.
Kwa
upande wake,mtaalamu huyo, amepongeza mfumo wa uendeshaji wa biashara
wa Kampuni ya JATU PLC na kuongeza kuwa mfumo huo utakuwa madhubuti
zaidi endapo utasimamiwa vizuri.
Ameongeza
kuwa katika siku 14 atakazokuwa hapa nchini kama sehemu ya jopo la
washauri atahakikisha kampuni hiyo inafikia malengo ya uanzishwaji wake
Kwa kufikia hatua nzuri itakayotatua changamoto zote kibiashara kwa
kuboresha uwekezaji wake.
Nae,
Mwenyekiti wa Bodi ya JATU PLC, Mhandisi Dkt. Zaipuna Yonah
amewaondoa hofu Watanzania juu ya kampuni hiyo na kusema kuwa mabadiliko
makubwa ya uongozi yaliyofanywa mwezi Agosti mwaka 2022 yatahakikisha
maono ya kampuni hiyo yanafanyiwa kazi kwa weledi mkubwa.
No comments:
Post a Comment