Na Mwandishi Wetu
Mara baada ya kikosi cha Timu ya KMC FC kurejea Jijini Dar ea salaam jana, uongozi umetoa mapumziko ya siku nne kwa wachezaji na kwamba watarejea kambini Jumamosi ya Januari saba kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo mwingine dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Januari 13 katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni imerejea jana ikitokea Mbarali mkoani Mbeya ambapo ilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara dhidi ya Ihefu uliopigwa Januari tatu na kupoteza kwa goli moja kwa sifuri.
Wachezaji wa KMC FC wamepewa mapumziko hayo wakati huu Ligi ikiwa imesimama kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi na kwamba Jumamosi ya Januari saba Timu itaanza mazoezi ramsi kwa ajili ya mchezo huo ambao itakuwa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar.
" Tunakwenda kwenye mapumziko mafupi wakati huu ligi ikiwa imesimama, tumetoka kupoteza mchezo muhimu ugenini lakini bado tupo kwenye kiwango kizuri na kwamba baada ya Timu kurejea, Kocha Mkuu Thierry Hitimana na wasaidizi wake watafanyia kazi mapungufu waliyoyaona na hivyo kuendelea kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja.
Kwaupande wa hali za wachezaji, bado kunachangamoto ya wachezaji watano ambao wanamajeraha ambapo kati ya hao wachezaji watatu ni majeruhi wapya waliotokana na mchezo uliopita dhidi ya Ihefu huku wawili niwale wamuda mrefu.
Majeruhi wapya ni Baraka Majogoro, George Makang'a pamoja na Ibrahimu Ame huku wale wamuda mrefu ni Hance Masound Msonga pamoja na Emmanue Mvuyekure ambapo wote wanaendelea na matibabu.
No comments:
Post a Comment