January 05, 2023

Maofisa Jeshi la Tanzania, askari walinda amani wakumbushwa wajibu wao


Mkuu wa Kanda ya Magharibi General ZARRER HAIDER akiwa na Mkuu wa Kikosi TANBAT 6 Luteni Kanali  Amini Stephen Mshana baadae ya kuwasili kikosini hapo akifanya ukaguzi.

 

Na Mwandishi Wetu

Maofisa wa Jeshi la Tanzania na askari walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha sita kutoka Tanzania wametakiwa kuwa makini  na mabomu ya ardhini yanayotengenezwa na vikundi vya waasi Afrika ya Kati.

Aidha maofisa hao wamekumbushwa wajibu wao hasa wa kufahamu ni wakati gani watatumia nguvu wakati wanapoendelea na majukumu ya yao ya kulinda amani huko Afrika ya Kati.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Mkuu wa Ujumbe wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kanda ya Magharibi (MINUSCA) Brigedia Jenerali Zarrer Haider wakati alipofaya ziara katika kambi ya walinda amani hao iliyopo Afrika ya kati kati Mkoa wa Beriberati Mambele kadei.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa habari wa kikosi hicho Kapteni Mwijage Inyoma alisema Brigedia Haider amewakumbusha walinzi wa amani kuendeleza kazi nzuri ya ulinzi wa amani ikiwemo kuendeleza ushirikiano na taasisi za dini, afya na wadau wengine wa ulinzi wa amani ndani ya MINUSCA.

"Ni muhimu kuzidi kung'ara kama mnavyoonyesha  umakini kwenye kazi za ulinzi wa amani , hata hivyo mnapaswa kuwa makini na mabomu ya ardhini yanayotengenezwa na vikundi vya waasi pia mfahamu ni wakazi gani mnapaswa kutumia nguvu," alisema Brigedia Haider katika taarifa hiyo.

Aidha maofisa na walinda amani hao wametakiwa kuendelea kuwa makini na ugonjwa wa Uviko-19 na malaria ili watekeleze majukumu yao ya ulinzi wa amani kwa ufasaha zaidi.

Akitoa shukrani kwa niaba ya kikosi hicho, Mkuu wa kikundi hicho Luteni Kanali Amini Mshana alisema kuwa amepokea  maelekezo ya mkuu huyu na ana budi kuyafata na ameahidi kikosi chake kitaendelea kuwa na ushirikiano kwa wananchi wanaowalinda na wadau wa Umoja wa Mataifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Pages