Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kampuni
ya Bima ya Sanlam General Insurance imezindua kampeni kabambe kwa
mawakala wake ambapo washindi watajinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo
Gari, Bodaboda na zingine nyingi kupitia Program ya Vuna Point.
Akizungumza
jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi huo Meneja Masoko na
Maendeleo ya Biashara, Matawi na Mawakala wa kampuni hiyo, Charles
Magori amesema lengo la kuanzishwa kwa tuzo hizo ni kutoa hamasa kwa
mawakala wa kampuni hiyo pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
"Lengo
kubwa la kuanzishwa kwa Tuzo hiI ni kutambua mchango wa mawakala wetu
sambamba na zitawasaidia kuongeza ufanisi na ubunifu zaidi katika
kutoaji wa huduma zao hivyo kupelekea kukua kwa mtandao wa biashara zao"
Alisema Bw. Magori.
Amebainisha
kuwa kampuni hiyo ambayo ina mtandao mkubwa wa mawakala ambao
wanapatikana katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Mbeya,
Arusha, Dodoma, na Mbagala, Zanzibar na pia wanataraji kufungua mkoani
Morogoro.
Katika
hatua nyingine, Magori ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kujiunga
kuwa wakala wa kampuni hiyo kujitokeza kwa wingi ambapo ameeleza kuwa
wanachotakiwa kufanya ni kupiga simu kupitia namba 0800750236 na
kusajiliwa kuwa wakala.
Kampuni
ya Bima ya Sanlam General Insurance ina uzoefu wa zaidi ya miaka 40 ya
utoaji wa huduma za bima na soko la bima nchini imekuwa ikitoa huduma
za Bima za Watu na Bima za biashara.
No comments:
Post a Comment