January 24, 2023

TANBAT 6 wawashauri wananchi Afrika ya Kati kuilinda amani, kukomesha migogoro


Mkuu wa wilaya ya Mambere kadei akimkaribisha mmoja wa wawakikosi kutoka TANBAT6 baada ya kufika kwa ajili ya kuungana na wananchi ili kutatua mgogoro wa wakulima na wafugaji.



Na Janeth Jovin

KIKOSI cha sita cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania (TANBAT 6), kimewashauri wananchi kijiji cha Sapuoa kilichopo kilometa 37 kutoka Mjini Beriberati nchini Afrika ya Kati,  kuilinda amani waliyonayo na kukomesha migogoro ya mara kwa mara.


Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa habari wa kikosi hicho, Kapteni Mwijage Inyoma alisema kijiji hicho hapo awali kilikuwa na migogoro baina ya wakulima na wafugaji haki iliyotishia amani lakini tangu kilipokuja kikosi cha TANBAT 6 kimefanikiwa kukomesha tatizo hilo.


Alisema walinda amani kutoka Tanzania wanaendelea kuwashauri wananchi wa kijiji hicho kushirikiana kwa umoja na kupendana ili kuleta maendeleo na kuendeleza amani ambayo inazidi kujengeka nchini mwao.


"Kijiji cha Sapuoa kilikuwa katika mgogoro wa muda kati ya wakulima na wafugaji kwa kuibiana mifugo na wakulima kuhalibiwa mazao, hali liyosababisha wadau wa walinda amani kusaidia kuondoa mgogoro huo kwa kuwakutanisha na kufanya mazungumzo yaliyoleta muafaka wa mgogoro huo," alisema Kapteni Inyoma katika taarifa yake


Aidha alisema walinda amani wa UN kutoka Tanzania katika utekelezaji wa jukumu la kuimalisha mahusiano na upendo kati ya wananchi wa Afrika ya kati wanaendelea na mikakati wa kuunga mkono wadau wa Umoja wa Màtaifa MINUSCA kwenye kuhamasisha amani katika vijiji mbalimbali mkoani Beriberati, Mambele kadei.


Kwa upande wake kiongozi wa Kijiji hicho cha Sapuoa, And Darius alisema anawashukuru walinda amani wa Tanzania kwa kazi wanazofanya hasa za kuhakikisha amani inapatikana wakati wote eneo hilo.


Alisema walinda amani hao  wamesaidia kuwakutanisha na kuondokana na mgogoro ambayo ulikuwa na sura mbaya kwenye jamii yao.


"Hakika Walinda amani kutoka Tanzania chini ya Umoja wa Màtaifa (UN) wanatujali sana na lazima tuendelee kuwaunga mkono katika kazi zao za ulinzi wa amani hapa nchini kwetu Afrika ya Kati," alisema

No comments:

Post a Comment

Pages