Mamlaka
ya Mapato Nchini (TRA) imewataka Watanzania kuendelea kutoa taarifa
pale wanapoona kuna vitendo vya udanganyifu (magendo) vinavyofanyika
hasa katika Maeneo ya Fukwe za Bahari,bandarini kwenye fukwe za Maziwa
pamoja na Mipakani.
Aidha,
mamlaka hiyo imewataka maafisa wake kujiendeleza kielimu kwa kutumia
fursa masomo zilizopo kwenye Chuo cha Kodi cha TRA ili kujiimarisha
kiutendaji pamoja na kuiongezea nchi mapato.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Fedha wa Mamlaka hiyo, Dinah Edward
akimwakilisha Kamishna Mkuu wa Forodha wa TRA, Alphayo Kidata wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Forodha Duniani ambayo hufanyika
Januari 26 kila mwaka ambayo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Amesema
kuwa wananchi wakishiriki kikamilifu kutoa taarifa hizo kutasaidia
kupunguza matukio hayo na kuisaidia TRA kuweza kukusanya ushuru na kodi
za Serikali.
"
Wananchi waendelee kutoa taarifa wanapoona watu wanaofanya vitendo vya
magendo na udanganyifu wakifanya hivyo watatusaidia kukusanya mapato ya
Serikali," amesema Dinah.
Amesema
kuwa TRA imekuwa ikijikita katika kuhamasisha wafanyabiashara kulipa
kodi hivyo kukwepa kodi ni kinyume cha sheria na kanuni za Serikali.
Pia
amesema siku hiyo imewekwa kwa ajili ya kuwaweka pamoja wanachama wa
Wakala Wa Forodha ili kuangalia kwa pamoja fursa zilizopo duniani pamoja
na kuona namna ambavyo mataifa mbalimbali yanafanya shughuli kwa uwiano
sawa.
Katika
hatua nyingine, Mkurugenzi huyo amewahimiza mawakala wa forodha nchini
kujiendeleza kitaaluma ili kuendana na miongozo, sheria na kanuni za
kidunia za taaluma hiyo.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Forodha wa TRA, Said Athman amesema katika
kutekeleza mkataba wa kimataifa wa Wakala wa forodha tayari serikali
imeanza kunufaika na biashara za kimataifa pamoja na kukuza pato la
Taifa kupitia kodi.
Akizungumzia
kuhusiana huduma mbalimbali zinazotolewa na TRA, amesemema kuwa Mamlaka
hiyo ni nambari moja kwenye ubunifu, Automation na ufuatiliaji.
“Tumeimprove
njia za ukusanyaji Mapato katika vituo mbalimbali vinavyotolewa huduma
na TRA ikiwa na huduma za kijamii, Sisi wakala wa Forodha umetupatia
Access za kuingia kwenye mifumo na kufanya Return Assessment.” Ameeleza
Nae,
Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Nchini, Edward Urio, ameiomba TRA
kuwashirikisha walipa kodi katika utekelezaji wa mujukumu yao ili
kuondoa kodi kinzani kwa wazalisha wa bidhaa mbalimbali.
Shirikisho
la Wakala wa Forodha Duniani lilianzishwa mwaka 1952 Nchini Ubelgiji,
Tanzania ilijiunga mwaka 1964 lengo ni kujiweka katika nafasi za
kimataifa ili kunufaika na misaada pamoja na mafunzo, misaada,
ushirikishwaji, pamoja na vikao vinavyofanyika kimataifa.
No comments:
Post a Comment