Na John Richard Marwa
Wakati joto la pambano la kufa ama kupona Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC hatua ya makundi kunako kundi D Young Africans dhidi ya US Monastiry, Mashabiki wa takiwa kujitokeza kwa wingi kwenda kuwapa Nguvu wachezaji wao.
Hayo yamebainishwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ali Kamwe, amesema Mashabiki wajitokeze kwa wingi huku wakiwa na lengo la kwenda kushangilia muda wotebna sio kwenda kushangilia matukio na kutumia muda mwingi wa kuji 'Snap'.
"Niwaambie mashabiki wa Young Africans Silaha yetu ni mchezaji wa 12 kwa maana ya mshabiki. Jukumu letu ni kuujaza Uwanja kwani wapinzani wetu baada ya kutua Kocha wao aliuliza Benjamin Mkapa itajaa na akaambiwa itajaa, ni kama wameingia upepo kwaiyo ni jukumu letu sisi kwenda kumalizana nao.
"Kikosi chetu kiko salama na jambo zuri ambalo wapenzi na mashabiki huwa wanataka kusikia ni kuwa wachezaji wote wako salama. Majeruhi waliopo wanaendelea vizuri, Aboutwaribu Mshery ameanza kutembea bila magongo na Bernard Morrison leo ama kesho atajiunga na kikosi kwa ajili ya mazoezi." Ali Kamwe ameongeza kuwa.
"Tunaingia kwenye huu mchezo tuna mambo matatu ya kumalizana na na Monastiry kwanza kushinda, pili kulipa kisasi cha mabao mawili waliyotufunga kwao na tatu ni kuwazuia wasiwe kama Raja Casablanca ambao hawataki kupoteza mchezo wowote kwenye hatua ya makundi." Pia Ali Kamwe amesema..
"Tunaamini kabisa Monastiry haji Dar es Salaam kukamilisha ratiba wanakuja kutafuta rekodi, kwamba mwaka fulani tulifanya vizuri na tulikuwa na rekodi bora, hilo tunalifahamu na tumechukua tahadhali zo te dhidi ya hao jamaa" amesema Kamwe
Yanga watashuka dimbani Benjamin Mkapa jumapili hii kuwakabili miamba ya kundi lao US Monastiry kutoka Tunisia siku ya jumapili mtanange unatarajiwa kulindima majira ya saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment