Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Balozi
wa Marekani Nchini Tanzania Michael Battle anatarajia kuwa Mgeni rasmi
katika Hafla ya Kifungua Kinywa kwa Wanawake( Accelerates Executive
Women's Breakfast) itakayofanyika Machi 18 mwaka huu katika Hoteli ya
Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na wanahabari jijini humo Mkurugenzi wa Kampuni ya Accelerate Business
Group Bernice Fernandes amesema kuwa lengo la hafal hiyo katika
kuwaezesha wanawake ni kutoa fursa kwa watendaji, wajasiriamali na
viongozi wenye mawazo ya kitalaam kwa mtandao wa kubadilishana mawazo
juu ya uwezeshaji wa wanawake.
Ameyataja
malengo mengine ni wanawake kujifunza kutoka kwa viongozi wazoefu
waliofanikiwa, kujadili mikakati ya kuvunja vikwazo vinavyokwamisha
maendeleo ya wanawake na kutambua fursa za kusaidia mipango ya
kuwezesha.
" Tunafurahi kuwashikilia wanawake
hawa mashuhuri amabao wamevunja dari katika kazi zao. kama mwanamke ni
muhimu kuungana na kushirikiana katika mafanikio tuliyoyapata. Pia
inatia moyo kusikia safari za wanawake hawa katika nafasi zao za
uongozi," amesema Bernice.
Amesisitiza kuwa
hafla hiyo itatoa ufahamau na msukumo mkubwa kwa washiriki wote katika
kuchangia sababu za uwezeshaji wa wanawake katika jamii kufikia malengo
ambayo wanayatamani.
Kwa upande wake, Mjumbe
Mtenfdaji wa Kampuni hiyo, Teddy Chamshama, amewahimiza wanawake kushiri
hafla hiyo ikatayoanza kuanzia Saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana kwani
watapata fursa ya kubadilshana mawazo na wanawake watendaji wa makampuni
waliofanikiwa.
Chamshana amefafanua kuwa
wanawake wanaohitaji kuhudhuria hafla hiyo wanatakiwa kufuatilia kurasa
za mitandao ya kijamii ya kampuni hiyo na kupiga simu 0692818823 ili kujua utaratibu wa kupata tiketi au kufika hotelini hapo.
Nae,
Muuguzi kutoka Premier Care ambao ni sehemu ya wadhamini, Emma Kamande
amesema siku hiyo watatoa huduma za afya bila malipo na kwamba wanawake
watakaohudhuria watafanyiwa vipimo vya magonjwa ya presha, sukari pamoja
na upimaji uzito.
No comments:
Post a Comment