Na John Richard Marwa
Nyota Agustin Okrah na Ismael Sawadogo wataukosa mchezo wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL hatua ya makundi, kunako kundi C ambapo Simba atawaalika AC Horoya katika Dimba la Benjamin Mkapa Jumamosi ya wiki hii.
Simba wanashuka dimbani wakiwa wanahitaji ushidi pekee ili kutinga hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika misimu mitano iliyopita.
Wakati Simba wakihitaji ushindi pekee kwenye pambano hilo, wachezaji tayari wameingia kambini kujiandaa na mchezo huo hapa jana huku wakiweka bayana kuwakosa Okrah na Sawadogo ambao bado wanauguza majeraha yao.
Kwa mujibu wa Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Okrah ataendelea kukosekana pamoja na Sawadogo huku Kibu Denis amerejea kikosini.
"Agustin Okrah na Sawadogo wataukosa mchezo wetu dhidi ya Horoya, Okrah alivunjika kidole kwenye mchezo wa kirafiki dhidi Al Hilal ambapo alitarajiwa kurejea dimbani baada ya wiki nne lakini ndio ameanza mazoezi mepesi.
"Kwa Ismael Sawadogo nae atakosekana kwa sababu alipata majeraha ya nyonga hivyo nae ataendelea kukosekana na hatatakuwa sehemu ya kikosi kinachijiandaa kuwavaa Horoya." amesema Ahmed na kuongeza kuwa.
"Habari njema na njema tena ni urejo wa Kibu Denis ambaye yuko tayari na leo (Jana) anaingia kambini kuungana na kikosi cha maandalizi ya kwenda kumteketeza Horoya pale Benjamin Mkapa, lengo likiwa ni moja tu kwenye mchezo huu kutinga hatua ya Robo Fainali na si vinginevyo." Ahmed Ally.
No comments:
Post a Comment