• Aishukuru ORYX ENERGIES, FOMAC kwa udhamini
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amegawa mitungi ya gesi 700 kwa wanawake wajasiriamali 700 wa Mkoa wa Mwanza lengo likiwa ni kuhamasisha kuacha matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa na badala yake watumie nishati safi ili kuhifadhi mazingira.
Aidha Masanja amekabidhi fedha kiasi cha Sh. Milioni 21 kwa wajasiriamali hao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mitungi hiyo ya gesi jana katika Ukumbi wa Rocky City Mall jijini Mwanza, kwa niaba ya Masanja, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Reuben Jichabu amewataka wanawake hao kutumia nishati ya gesi ya ORYX katika shughuli zao za ujasiriamali na kuepuka matumizi ya kuni.
Naye, Masanja ameahidi kuendelea kuwaunga mkono wajasiriamali wanawake wa Mkoa wa Mwanza ili waweze kukuza uchumi wao.
Pia, amezishukuru Kampuni za ORYX na FOMAC kwa kudhamini na kufanikisha tukio hilo.
No comments:
Post a Comment