March 23, 2023

SHEIKH MKOA WA SINGIDA, AOMBA SERIKALI KUTOKOMEZA MADANGURO MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro, akizungumza wakati akifunga mafunzo ya wahitimu wa dini ya kiislam katika Madrasa ya Siraj i iliyopo Msikiti wa Kibaoni mjini hapa hivi karibuni.


Na Dotto Mwaibale, Singida


SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro ameuomba uongozi wa Mkoa wa Singida kuyatokomeza madanguro na vijiwe vyote vya wanawake wanaojiuza kuhakikisha vinavunjwa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Sheikh Nassoro alitoa ombi hilo mwishoni mwa wiki wakati akifunga mafunzo ya wahitimu wa dini ya kiislam katika Madrasa ya Siraj i iliyopo Msikiti wa Kibaoni mjini hapa.


"Kwa heshima hii ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani naiomba Serikali ya Mkoa wa Singida, kuhakikisha madanguro yote yaliyopo mkoani Singida yanatokomezwa" alisema Nassoro.


Katika hatua nyingine Sheikh Nassoro amewataka waumini wa dini ya Kiislam mkoani hapa kuacha tabia ya kuwabeza, kuwadhalilisha na kuwashutumu walimu wa dini badala yake watambue thamani yao.


Alisema waislam wanatakiwa kutambua  kuwa walimu hao sio malaika bali ni wanadamu wanamapungufu kama ilivyo kwa watu wote na katika mapungufu hayo wachukue yaliyomema kutokana na adhi yao.


Alisema waimu hao wa dini wanafanya kazi kubwa sana katika madrasa mbalimbali tena katika hali duni, hawana posho huku mishahara yao ikiwa ni matusi, kudhalilishwa na kupewa maishaaaaa mabaya.


Sheikh Nassoro aliwaomba waislam kuanzia sasa kujenga utamaduni katika misikiti kuhakikisha linapatiana fungu la walimu hao wa madrasa.


Aidha, aliwataka walimu hao wa dini kuhakikisha wanasimamia maadili kwa watoto wa kiislam hasa katika kipindi hiki cha sasa ambapo dunia inawaangaza watoto wa kiume katika kuleta hadaa ya kuwagiribu ili wawe mabarazuri ;mashoga;


“Sinto pendezewa, sinto furahi, sintosikia amani kusikia moja ya madrasa kuna watoto ambao ambao wameanza kuwa mabarazuri” alisema Nassoro.


Sheikh Nassoro pia alisema masheikh wa kata ndio wasemaji wa kuu wa waisalam    katika kata zao hivyo wanatakiwa kuwasemea waislam na kuupigania uislam na si vinginevyo.


Alisema hivi sasa wanaingia katika kipindi cha mafungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani moja ya wajibu wao ni kujua idadi ya waislam waliopo kwenye maeneo yao hasa watu wenye mahitaji maalumu wakiwepo mayatima jambo litakalosaidia kuwapatia misaada ya kibinadamu.

No comments:

Post a Comment

Pages