HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 21, 2023

SMZ, Sinotec wasaini mkataba Mradi wa Nyumba za Maendeleo


Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (WAMM) Dkt. Mngereza Mzee Miraji (kushoto) na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya SINOTEC Jin Hua (kulia) wakisaini hati ya Makubalino (MoU) ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Maendeleo Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa WAMM Maisara, Unguja.

 

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (WAMM) imesaini hati ya makubaliano na kampuni  ya Sinotec kwa ajili  ya Mradi wa Nyumba za Maendeleo Zanzibar.
 

Hafla ya utiaji saini  imefanyika jana katika ukumbi wa wizara hiyo ambapo kwa upande wa Wizara alisaini Katibu Mkuu Dkt Mngereza Mzee Miraji na kwa kampuni ya Sinotec alisaini Naibu Meneja Mkuu Jin Hua.

Akizungumza mara baada ya utiaji wa saini hiyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mngereza amesema makubaliano hayo ni hatua ya mwanzo  katika utekelezaji wa mradi huo, ambapo lengo kuu ni kutekeleza Sera ya Makaazi bora kwa wananchi kupitia wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar.

Naye Naibu Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Jin Hua amesema amefarajika kupata fursa hiyo ya Kufanya kazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Ardhi ili kuifanya jamii kuwa na Makaazi bora ya kuishi.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) Mwanaisha Ali Said amesema ujio wa kampuni hiyo ni faraja kwa Serikali kwani ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Maendeleo utaweza kuondoa uhaba wa nyuma Zanzibar.   

 

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar inaendelea na hatua mbali mbali za utiaji saini ya miradi ya Ujenzi wa Nyumba za Maendeleo ambapo awali ilitiliana saini na kampuni ya ASER Construction and Technology Ltd.

No comments:

Post a Comment

Pages