Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Wakazi
wanaotakiwa kuhama katika Bonde la Mto Msimbazi wametakiwa kuwa
watulivu kwamba kila mtu anayestahili atalipwa fidia yake.
Hayo
yamesemwa na Mratibu wa Miradi ya DMDP pamoja na Mradi wa Kuendeleza
Bonde la Mto Msimbazi Mhandisi Humphrey Kanyenye akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi baada ya
kuibuka kwa baadhi ya wakazi hao kulalamika kwamba fidia ni ndogo.
Mhandisi
Kanyeye amesema kuwa Serikali haipo tayari kumdhulumu mtu yeyote haki
yake, hivyo kama kuna mtu mwenye malalamiko anatakiwa kuyaripoti kwenye
dawati la malalamiko ili yafanyiwe kazi.
“Kama
kuna malalamiko yapelekwe kwenye dawati la malalamiko na utasikilizwa,
na kama hutaridhika nenda mahakamani, lakini kulalamika kiholela ni
kuleta taharuki,” amesema Mhandisi Kanyeye.
Amebainisha
kuwa kwa sasa wanaendelea na uhakiki wa thamani zinazoathirika na mradi
huo ili kujua gharama ya fidia ambayo kila mtu anastahili kulipwa.
Kwamba
katika zoezi hilo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya wananchi
wamashafanyiwa uthamini wa mali zao na wamekubaliana na fidia
walizowekewa na wapo wachache waliokataa, lakini wanaendelea
kushughulikia jambo hilo.
“Kimsingi
walitakiwa wasilipwe kwani walishapewa notisi tangu mwaka 1979
kwasababu eneo hilo ni hatarishi, lakini Serikali kwa kujali imeamua
walipwe, hata hivyo hatuwezi kulipa kitu ambacho hakipo,” amebainsha
Mhandisi Kanyenye.
Mhandisi
Kanyeye amesisitiza kuwa wanalipa thamani ya mali iliyopo kwa sasa na
sio vinginevyo na kueleza kuwa wao baadhi ya wananchi wenye matarajio
makubwa kuliko uhalisia.
No comments:
Post a Comment