RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinwarakiwa yi amewahimiza watafiti kuhakikisha tafiti zao zinawafikia watumiaji.
Pia Dk. Mwinyi alishauri matokeo ya utafiti yawafikie watunga sera ili wayatumie kwa utungaji wa sera bora.
Dk.
Mwinyi ameyasema hayo kwenye hafla ya kusambaza matokeo ya tafiti za
UVIKO-19 zilizofanywa na chuo Kikuu cha MUHAS kupitia ufadhili wa
familia ya Hayati Amne Salim hafla iliyofanyika kwenye jengo la CHPE,
kampasi ya Muhimbili Dar es Salaam.
Dk. Mwinyi aliwataka wataalam wa ndani kuyapokea matokeo ya utafikti huo na
kuyafanyiakazi, ili kuongeza kasi ya udhibiti wa maambikizo ya UVIKO -19 nchini.
Alieleza
tafiti hizo zimeonesha namna za athari za ugonjwa huo na kuongeza kuna
mafunzo yakitumiwa vyema yatasaidia mapambano sio tu ya UVIKO bali pia
kwa magonjwa mengine.
"Bila shaka ushauri WA
kisayansi unaweza kuwa na tija zaidi ikiwa utatumika kwa wakati na sio
kukaa kwenye majarida ya kimataifa peke yake" Alishauri Dk. Mwinyi.
Alisema
msaada uliotolewa na familia ya Hayati Mama Amne Salim, Mke wa Dk.
Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania unakumbusha jukumu la
kila Mtanzania popote alipo kwa namna yake kuona anamchango kwa taifa
lake.
"Kwa utaratibu huu tunaweza kwenda mbali zaidi na kupambana na hatari yoyote" Alieleza Dk. Mwinyi.
Aidha,
Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo, kuipongeza familia Hayati Mama
Amne Salim kwa niaba ya serikali zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Pia
Dk. Mwinyi alikipongeza Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) kwa kuutendea haki ufadhili huo na kueleza kuwa
taasisi ya MUHAS ilihakikisha Fedha zilizotolewa kwaajili ya utafiti huo
shilingi milioni mia moja na tano zilitumika kwenye utafiti huo.
"Nawapongeza
MUHAS kwa weledi na uadilifu wenu, utaongeza fursa zaidi za ufadhili wa
utafiti kutoka kwa Watanzania wengine" Alipongeza Dk. Mwinyi.
Pia
Dk. Mwinyi aliwawapongeza wanasayansi wa MUHAS na Watanzania kwa ujumla
kwa kazi nzuri wanazoendelea kuzifanya na kusifu kufarajika kwake kwa
chuo cha MUHAS kuwa cha kwanza Afrika Mashariki na Kati kufanya tafiti
nzuri na machapisho.
Alieleza kwamba anatarajia
tafiti hizo zitaleta unafuu kwa wananchi kwa kutatua changamoto
zinazoijabili jamii ili kufikia malengo endelevu nchi iliyojipangia.
Mapema
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda,
aliwataka wadau wajitokeze kufanya tafiti mbalimbali na waunge mkono
kazi iliyofanywa na Dk. Salim Ahmed Salim pamoja na familia yake.
Pia
alibainisha Serikali imetenga shilingi milioni 50 kwa kila utafiti
utakaofanywa na machapisho yake yakichapishwa sehemu mbalimbali duniani. IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment