April 11, 2023

Airpay waingia makubaliano na SMZ kuchangia dira ya Serikali ya 2050

 NA MWANDISHI WETU,  ZANZIBAR


KAMPUNI ya Airpay kutoka  India imeingia  makubaliano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuchangia katika dira ya serikali ya 2050 kwa lengo la kuongezea uelewa kuhusu uwezeshaji kidijitali kwa wafanyabiashara kupitia huduma zake mbalimbali.

Akizungumza hivi karibuni visiwani Zanzibar katika mkutano wa jumuiya ya wafanyabiashara, wawakilishi wa serikali wakiwamo wasimamizi na watunga sera, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Airpay,  Kunal Jhunjhunwala alisema wanajisikia furaha kuja na teknolojia yao kutoka India na kuingiza Tanzania katika visiwa vya Zanzibar.



Jhunjhunwala alisema teknolojia yao inalenga kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati katika kuingia kwenye biashara mtandao kwa kutumia simu zao za mikononi.


"Tunajisikia furaha kuja na teknolojia yetu kutoka India na kuingiza nchini Tanzania, naishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Tanzania bara kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia na tutatumia uwezo wetu kama mdau wa muda mrefu wa uwezeshaji kifedha kidijitali," alisema


Awali akifungua mktano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayejusika na Ajira, Masuala ya Uchumi na Uwekezaji, Mudrick Soraga alisema kwa mujibu wa tafiti za Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania imepiga hatua kwenye masuala ya uchumi shirikishi.


"Hata ripoti ya Benki ya Dunia imeeleza kuwa namba ya ushirikishwaji katika sekta ya fedha kwa watu wazima miaka 15 na zaidi iliongezeka kwa asilimia 52 mwaka 2021 kutoka asilimia 17 mwaka 2011. Hata hivyo, asilimia 48 ya watu wazima haijashirikishwa bado kwenye huduma rasmi za fedha ikiwemo pengo la kijinsia la  asilimia 13," alisema Soraga na kuongeza


"Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayo furaha kupokea teknolojia  mpya kutoka India inayolenga kutikiza azma ya serikali. Uamuzi wetu kuja zainzabar ni sahihi,na tunaona Nia njema za kushirikiana kufikia lengo la 2050,, alisema Soraga.


No comments:

Post a Comment

Pages