Na Victor Masangu, Kibaha
Jumuiya
ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Kibaha Mji katika
kuboresha afya ya mama na mtoto imeamua kufanya ziara katika kituo cha
afya mkoani kilichopo Wilaya ya Kibaha na kufanya matendo ya huruma
katika wodi ya wazazi kwa kugawa msaada wa vifaa mbalimbali na mahitaji
muhimu.
Akizungumza
wakati wa kutoa msaada huo Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya wazazi Yahaya
Mtonda amesema kwamba wameamua kufanya ziara hiyo ya kutembelea kituo
hicho cha afya ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya wazazi hivyo wakaona kuna
umuhimu kufanya matukio ya kuisaidia jamii.
Mwenyekiti
huyo ya wazazi ambaye aliambatana na viongozi mbali mbali wa jumuiya
hiyo wakiwemo wajumbe wa kamati ya utekelezaji sambamba na baadhi ya
madiwani ambapo walipokelewa kwa furaha na kuweza kupata fursa ya
kuwatembelea wazazi waliojifungua kwa ajili ya kuwajulia hali na
kuwapatia mahitaji yao muhimu wanayostahili.
Mtonda
alisema kwamba jumuiya yao ya wazazi imeona kuna changamoto mbali mbali
ambazo zinawakabili wakinamama wajawazito pindi wanapojifungua
wanahitaji mahitaji mbali mbali ili kuweza kuwasaidia pindi wanapokuwa
wodini wao pamoja na watoto ambao wamezaliwa.
"Tupo
katika kipindi cha maadhimisho wiki ya wazazi ambapo kwa Upande wetu
kama Wilaya ya Kibaha mji tumeamua kuchagua baadhi ya maeneo kwa ajili
ya kuyatembelea ikiwemo kituo Cha afya mkoani hususan katika wodi ya
wazazi na tumetoa msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo sabuni,pampasi za
watoto pamoja na mahitaji mengine muhimu kwa ajili ya watoto na
wakinamama.
Aidha
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kubadilika kwa
kuhakikisha kwamba wanawalea na kuwatunza watoto wao kwa lengo la
kuijenga nchi na kwamba wataendelea kushirikiana na Serikali katika
kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazokikabili kituo hicho ikiwemo
kuboresha miundombinu ya majengo ili wagonjwa waweze kupata huduma
nzuri.
Awali
mganga mfawadhi wa kituo cha afya Mkoani Abdulkadri Sultan ameipongeza
kwa dhati jumuiya hiyo ya wazazi kutokana na kuona umuhimu mkubwa wa
kutumia wiki ya maadhimisho yao kwenda kutoa msaada katika wodi ya
wazazi kwani wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mahitaji
pindi wanapojifungua.
Sultan
alisema kuwa licha ya jumuiya ya wazazi kwenda kutoa msaada lakini kwa
Sasa bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kupokea idadi
kubwa ya wagonjwa ukilinganisha na idadi ya wodi zilizopo ni chache
hivyo kuiomba jumuiya hiyo iwasadie katika jambo hilo.
Naye
diwani wa Kata ya Tumbi ambaye naye alishiriki katika ziara hiyo
hakusita kuwashukuru kwa dhati uongozi mzima wa jumuiya ya wazazi Wiyala
ya Kibaha mji kwa kuona umuhimu wa kuwasapoti kwa hali na mali
wakinama hao pamoja na watoto wao.
Nao
baadhi wa wakinamama ambao walipata fursa ya kutembelewa na kupatiwa
msaada wa vitu mbali mbali wamesema kitendo hicho kimeweza kuwafariji
kwa kiasi kikubwa kwani hawakuweza kutegemea kama watapatiwa msaada huo
kwani utawasaidi wao pamoja na watoto wao.
Katika
hatua nyingine uongozi wa jumuiya hiyo uliweza kutoa salamu zao kwa
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka pamoja na mke wa Mbunge
Selina Koka kwa kuweza kusapoti kufanikisha zoezi hilo pamoja na wadau
wengine wakiwemo baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji Kibaha.
No comments:
Post a Comment