Na Victor Masangu, Kibaha
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kibaha Mji Ramadhani Kazembe amewataka vijana wenzake kuhakikisha wanashikamana kwa pamoja na kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuchapa kazi kwa uzalendo ili kuleta chachu ya maendeleo.
Kauli
hiyo ameitoa wakati wa ziara yake katika kata ya Tangini yenye lengo la
kuweza kuzungumza na vijana pamoja na kutoa shukrani zake za dhati kwa
kuweza kumchagua kushika nafasi hiyo ya Mwenyekiti.
Mwenyekiti
huyo alisema kwa sasa suala la uchaguzi limeshamalizika hivyo hakuna
budi kuachana kabisa na makundi na kuelekeza nguvu zao zote katika
kuweka misingi imara kuanzia ngazi za matawi hadi ngazi ya Wilaya ikiwa
sambamba na kutenda haki.
Aidha
katika hatua nyingine Mwenyekiti Kazembe amesema lengo lake kubwa ni
kuendelea kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo kwa kushirikiana na
vijana wenzake ili kuweza kuleta chachu ya maendeleo katika jumuiya ya
vijana.
Pia alifafanua
kwamba ataendelea kuwatumikia na kuwaongoza kikamilifu vijana wenzake
katika kutekeleza majukumu yake kwa weledi kwa kuzingatia kanuni ya
umoja wa vijana Kama inavyoelekeza katika ibara ya saba na nane kwa
lengo la kuongeza ufanisi zaidi.
Kwa
upande wake Katibu wa Uvccm Kibaha mji Gamalu Makona amesema kwamba
ataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wenzake pamoja na
vijana ili kuweza kuimarisha jumuiya ya umoja wa vijana.
Ziara
ya Mwenyekiti wa UCCM Wilaya ya Kibaha mjini katika kata ya Tangini
imeweza kuleta tija zaidi kwa jumuiya hiyo kutokana na kujadili Mambo
mbali mbali kwa maslahi mapana ya vijana pamoja na jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment