SHIRIKISHO la Riadha Barani Afrika CAA), limeanza vikao vyake jijini Lusaka Zambia, likishirikisha nchi wanachama ikiwamo Tanzania.
Tanzania inawakilishwa na Rais wa Shirikisho la Riadha (RT), Silas Isangi, ambaye anashiriki mkutano mkuu unaofanyika kwa siku mbili, Aprili 26 hadi 27.
Katika mkutano huo, kutajadiliwa mambo mbalimbali yatakayohusu maendeleo ya CAA na nchi wanachama.
Baada ya mkutano huo, shughuli zitahamia katika mji wa Ndola, ambako kutarindima michuano ya vijana chini ya miaka 18 na 20, kuanzia Aprili 29-Mei 3 ambapo Tanzania itawakilishwa na kikosi cha wanariadha 15.
Kikosi hicho cha wanaradha 15 chini ya Makocha Alfredo Shahanga na Asha Abdallah Khatib, kiko jijini Mbeya hivi sasa ambapo kiliweka mapumziko na leo Aprili 26 kufanya mazoezi mepesi kwenye Uwanja wa Sokoine.
Msafara wa timu, kesho Aprili 27 utaendelea na safari ukitumia basi maalumu lililotolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), na kuwasili siku hiyo hiyo Ndola tayari kwa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment