April 20, 2023

Wafanyakazi Benki ya CRDB wawakumbuka watoto Yatima

 Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu (kushoto) wakisaidiana kushusha baadhi ya vitu walivyokabidhi katika Kituo cha Kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga kilichopo Kinondoni Moscow jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu (kushoto) wakisalimia na watoto wa kituo hicho.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (wa pili  kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga, Zainabu Bakari, sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo unga, sukari, sabuni na mafuta vilivyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu. Hafla hiyo ilifanyika kituoni hapo Kinondoni jijini Dar es Salaam Aprili 20, 2023.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (wa pili kulia) akimkabidhi mtoto Fahad Best msaada wa begi la shule wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea Kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga na kukabidhi wa vitu mbalimbali vikiwemo unga, sukari, sabuni na mafuta. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kituo hicho, Zainabu Bakari. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu na wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Magomeni, Asha Ramadhani. Hafla hiyo ilifanyika kituoni hapo Kinondoni jijini Dar es Salaam Aprili 20, 2023.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya keki Mwenyekiti wa Kituo hicho, Zainabu Bakari.

Picha ya pamoja.


No comments:

Post a Comment

Pages