Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani akizungumza wakati alipotembelea mabanda mbalimbali.
Na Oscar Assenga, TANGA
KAIMU
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma
Ramadhani leo amewaongoza wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
kwenye maaadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani ambapo kilele chake
kitafanyika Mei 12 Jijini Mwanzasiku ya wauguzi Duniani.
Maadhimisho
hayo yalianza na maandamano kutoka eneo la Toyota mpaka Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kulipofanyika kilele cha maadhimisho hayo
Akizungumza
wakati wa maadhimisho hayo,Dkt Juma alisema kutokana na uwepo wa
changamoto ya usafiri kwenye mkoa huo ambayo ilielezwa wakati wa risala
ya wauguzi hao alieleza mipango ya uongozi wa hospitali hiyo kwenye
bajeti zijazo na jitihada walizoweka kama taasisi wana mpango wa kununua
basi.
“Kwa
sasa Hospitali kwenye bajeti zijazo na jitihada tulizowekeza taasisi
wana mpango wa kununua basi kwa ajili ya hospitali “Alisema Kaimu
Mganga Mfawidhi Dkt Juma.
Awali
akisoma risala hiyo Katibu wa Tana Tawi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Tanga Mwanaisha Nyangasa alisema maadhimisho hayo ni kutafakari na
kufauta nyayo za mwanzilishi wa huduma za uuguzi na ukunga Bi Florence
Night Ngare.
Alisema
wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wamemuenzi kwa
kutoa huduma mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo ikiwemo za uchunguzi
wa saratani ya kizazi na matiti kwa wakina mama ,uchunguzi wa kisukari
na macho,shinikizo la damu,kuhamasisha uchangia damu ,upimaji wa VVU kwa
hiari na sambamba na utoaji elimu ya afya na lishe kwa wateja
mbalimbali
Aidha
alisema pia katika maadhimisho hayo wametoa chanjo za Covid 19 ambapo
wananchi waliohudumiwa tokea walipoanza maadhimisho hayo ni 154 ambao
walihudumiwa kwa siku moja.
Hata
hivyo alisema kwamba Ukunga ni kada muhimu sana katika kufanikisha
utoaji wa huduma nzuri za afya kwenye jamii na unapozungumzia afya bora
muuguzi ni sehemu sahihi ya kufanikisha kila mtanzania anakuwa na afya
bora.
Alisema
kwamba pamoja hayo kuna mafanikio makubwa ikiwemo mazingira ya kufanyia
kazi yameboresha na miundombinu ya hospital na kuwezesha wanafanyakazi
kufanya kazi kwenye mazingira mazuri.
Aidha
alisema kwamba pia ni wauguzi kupata nafasi ya kujiendeleza
kimasomo,wauguzi kupata motisha mbalimbali,kuongezeka kwa hamasa kwa
wauguzi .
Akizungumzia
changamoto wanazokabiliana nayo alisema kwamba changamoto kubwa ni
upungufu wa watumishi idara ya ukunga na uuguzi kulingana na mahitaji ya
jamii kutokana na kuongezeka kwa vitengo na idara ambazo wauguzi
wanahitajika.
No comments:
Post a Comment