May 05, 2023

Mama Selina Koka awakumbuka wajane kwa vitendo awapiga jeki ya mitaji

 

Na Victor Masangu, Kibaha 

Mlezi wa jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Selina Koka katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa wanawake kiuchumi ameamua kutoa kiasi cha shilingi milinioni 22.8 ili kuwawezesha katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuwapatia mitaji na vitendea kazi.
 Selina ambaye pia ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji amebainisha kwamba ameamua kuwasaidia wanawake wa UWT Kibaha mji hasa wale wajasiriamali  ili waweze kuanzisha biashara zao ndogo ndogo lengo ikiwa ni kujikwamua kiuchumi.

Mlezi huyo alisema anatambua katika jinbo la Kibaha mjini kuna idadi kubwa ya wanawake ambao ni wajasiriamali ndio maana akaamua kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwa kata zote 14 ikiwa pamoja na kuwapatia fedhaa baadhi ya kata ili waweze kufungua akaunti zao zitakazowasaida kutunza fedha zao.

"Tulikuwa katika ziara ya UWT na  nimepata bahati ya kuzunguka katika kata zote 14 za jimbo la Kibaha nikiambatana na Mwenyekiti lakini nimeweza kutoa mitaji ya aina mbali mbali ikiwemo fedha pamoja vitendea kazi vingine ambavyo vitawasaidia katika kazi zao,"alisema Selina.
Kadhalika alioneza kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wanawake wa uwt pamoja na wengine katika kuweka mipango madhubuti ya kuwapatia mitaji mbali mbali ikiwemo sambamba na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali lengo ikiwa ni kujikomboa kiuchumi.

Pia sambamba na hilo aliwakumbuka wanawake wajane wa kwa kuwapatia mitaji ya mradi wa sabuni na kuwahimiza wafanye biashara hiyo kwa ajili ya kuleta matokeo chanya katika kujipatia kipato ambacho kitawasaidia kuendesha familia zao.


"Natamani kuona katika siku za usoni hii mitaji mbali mbali ambayo ninaitoa kwa wanawake inakuwa na tija na endelevu zaidi na kwamba fedha hizi mzitumie vizuri katika kuanzisha miradi ya tofauti na ndio maana hata wajane wa kata ya visiga nimewaanzishia mradi wa kuuza sabuni za kufulia.
 Kwa Upande wake Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Kibaha mji amempongeza Mke wa Mbunge la Jimbo la Kibaha mji kwa juhudi zake  za  kuwapatia mitaji  ambayo itakuwa ni mkombozi katika maendeleo.


Nao baadhi ya wanawake wa UWT ambao wamepata fursa ya kunufainika na mitaji hiyo akiwemo Fatma Omary ametoa pongezi zake kwa mlezi wao Selina Koka pamoja na Mbunge wa jimbo la Kibaha mji kwa kuonyesha njia ya kuwakomboa wanawake katika kujikwamua kiuchumi.


No comments:

Post a Comment

Pages