TIMU ya Taifa ya Riadha kwa vijana chini ya miaka 18 na 20, imefanikiwa kuvuna medali ya pili kwenye mashindano ya Afrika, yanayoendelea kwenye dimba la Levy Mwanawasa nchini Zambia.
Medali hiyo imepatikana Jumanne Mei 2, 2023 kupitia mchezo wa kurusha Tufe 'Shotput', baada ya Samir Sululu (pichani) kushika nafasi ya tatu na kujitwalia medali ya shaba kwa upande wa U 18.
Hongera sana kwao na hii ni kutokana na mfumo bora ulioanzishwa na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), kushirikisha wataalamu mbalimbali wa ufundi ukiacha wale ambao wameteuliwa rasmi kufundisha timu.
Pongezi kwa Mwanaamina na Samir, Makocha wa timu Alfredo Shahanga, Asha Abdallah Khatib, Kocha mwalikwa mtaalamu wa mitupo kutoka JWTZ Abdallah Juma Abeid, Meneja Amani Ngoka, Daktari Cosmas Kapinga, Mkuu wa msafara Muhidin Masunzu, uongozi wote wa RT, BMT na Wadau wote.
Tunawatakia kila la heri vijana wengine waliosalia, nao wafuate nyayo hizo.
Mashindano hayo yaliyokata utepe Aprili 29 yanatarajiwa kufikia tamati Mei 3.
No comments:
Post a Comment