Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Nipe Fagio , Ana Rocha, ametoa wito kwa jamii kuchukua jukumu la usimamizi wa taka na uhifadhi majumbani ili kuzuia magonjwa ya kuambukiza.
Akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya usafi Duniani , Rocha amesema jukumu la kudumisha mazingira safi linanzia nyumbani, akihimiza jamii kuwa na maeneo maalumu ya kutupia taka hizo.
"Ulimwengu unaweza kuwa salama bila taka ikiwa tutachukua hatua haraka. Jukumu hili linaanza na sisi," alisema. "Hatupaswi kuchafua mazingira kwa kuzalisha taka bila kujua wapi pa kuzihifadhi vizuri."
Katika maadhimisho ya Siku ya USafi yaliyofanyika siku ya Jumamosi, ajenda ya ulimwengu ni kutokomeza taka, haswa chupa za plastiki zinazotumiwa mara moja, kwa kutekeleza sera bora na juhudi za kuelimisha jamii.
Zaidi ya watu milioni 60 kutoka nchi 191 tangu zimeadhimisha siku hiyo ikiwemo Tanzania.
Tangu mwaka 2018, Nipe Fagio limekuwa mstari wa mbele katika juhudi za kusimamia ajenda ya usafi hapa nchini.
Akizungumza katika ufukwe wa Selander Beach jijini Dar es Salaam wakati wa kufanya usafi katika fukwe hiyo na maeneo mengine mbalimbali , Rocha amtoa wito wa serikali kuhakikisha ajenda ya usafi inafanikiwa katika maeneo yote.
Mbali ya kusherehekea siku hiyo, Nipe Fagio pia imesherehekea miaka 10 toka kuanzishwa kwake.
Kupitia Nipe Fagio, Rocha amesema kuwa kila mwaka wanatoa ripoti ya mambo ya usafi na mazingira na huwashirikisha wadau muhimu na wapanga sera ili kusaidia uhifahi mzuri wa mazingira.
Amesema kuwa ripoti ya mwaka 2023 pia itajumuisha uchambuzi kamili wa miaka 10 ya ukusanyaji wa data.
No comments:
Post a Comment