September 06, 2023

Serikali ya Marekani Yatangaza Dola Milioni 15 Kusaidia Mifumo ya Chakula Barani Afrika

Leo katika Kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika jijini Dar es Salaam, Tanzania, Naibu Kiongozi Mkuu wa Shirika la USAID Isobel Coleman na Msaidizi wa Msimamizi wa Ofisi ya Ustahimilivu na Usalama wa Chakula Dina Esposito wametangaza uwekezaji mpya kusaidia mifumo jumuishi na inayostahimili chakula barani Afrika, zikiwemo dola milioni 15 za kutoa msaada unaolengwa kwa wanawake, wakulima wadogo, na wafanyabiashara wadogo na wa kati katika mifumo ya chakula barani Afrika. Uwekezaji huu ni sehemu ya ufadhili wa ziada kutoka serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Feed the Future ili shughulikia uhaba wa chakula na ongezeko la bei ya mbolea barani Afrika.

 

Msaada kwa wanawake katika kilimo biashara

Wakati wa kikao cha ufunguzi wa jukwaa linalo wakukutanisha wadau kuingia makubaliano ya kilimo biashara - Naibu Msimamizi wa shirika la USAID Bi. Coleman alitangaza uwekezaji wa dola milioni 4 katika Mpango maalum wa kuinua wanawake katika kilimo biashara kwa mfumo wa masoko ya kidigitali barani Afrika (VALUE4HER). Asilimia sabini ya biashara ndogo na za kati zinazomilikiwa na wanawake katika nchi zinazoendelea haziwezi kupata huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji yao - upungufu huu wa kifedha unasababisha kukosekana kwa usawa wa kijinsia. VALUE4HER, inayotekelezwa na AGRA, itasaidia biashara ya kilimo inayoongozwa na wanawake kutatuwa vikwazo hivi kwa kuwawezesha kujenga mitandao ya kibiashara, kuongeza mtaji, na kuungana na wanunuzi, wafadhili na watoa huduma wengine.

 

 

Kuimarisha uweza wa kustahimili mishtuko

Wakati wa mkutano wa Jukwaa kuhusu upatikanaji wa mbolea na afya ya udongo barani Afrika, Msaidizi na Msimamizi wa Ustahimilivu na Usalama wa Chakula Esposito alitangaza uwekezaji wa dola milioni 5 katika ‘Sustain Africa” mpango unaoratibu washirika wa sekta ya umma na binafsi kusaidia wakulima wadogo kupata mbolea ya bei nafuu, kuimarisha uwezo wa kustahimili mitikisiko ya mbolea kwa siku zijazo, na kuhakikisha uhakika na upatikanaji wa chakula chenye lishe. Kupitia USAID, programu hii itapanua na kuboresha uwezo wa kufuatilia mienendo ya bei ya mbolea na kuashiria msaada unapohitajika. Uwekezaji huu unawezesha USAID na washirika wake wa sekta binafsi kusaidia wakulima milioni sita katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kufanikisha kulima mazao, hata wakati wa kipindi cha mshtuko

 

 

Uwekezaji katika lishe

Wakati wa hafla ya kufunga siku ya kwanza ya Jukwaa, Naibu Kiongozi Mkuu wa Shirika la USAID Coleman alitangaza uwekezaji wa dola milioni 6, kwa ushirikiano na Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) na Usimamizi wa Uwekezaji wa Incofin, katika Kituo cha Ufadhili wa Chakula chenye Lishe (N3F). Kituo hicho cha N3F cha kwanza cha aina yake ni hazina ya uwekezaji ambao unayolenga moja kwa moja kuboresha mlo na lishe katika nchi zilizo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia ufadhili wa biashara ndogo na za kati zinazohusika na utoaji wa chakula cha bei nafuu, salama, cha asili  na chenye lishe. Mfuko huo pia unaweka kipaumbele kwa uwekezaji unaokuza usawa wa kijinsia na kutoa angalau asilimia 30 ya mikopo yote kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake au zinazoongozwa na biashara ndogo na za kati.

No comments:

Post a Comment

Pages