Katibu Mkuu wa Shiuma Taifa - Venatus Magayane akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa shiuma taifa Matondo Masanja akizungumza na wamachinga wilaya ya Iringa Mjini.
Mgeni rasmi Katika mkutano huo Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Michael Semindu akitoa neno.
Baadhi ya viongozi wa muda wa Shiuma wilaya ya Iringa wakikabidhiwa katiba ya Shiuma.
NA DENIS MLOWE, IRINGA
Shirikisho la Umoja
wa Wamachinga nchini (SHIUMA) kupitia katika mkutano uliofanyika mkoani
Iringa wa kuchagua viongozi wa masoko mkoani hapa wamemfukuza aliyekuwa
Naibu katibu Mkuu wa shirikisho Hilo Joseph Mwanakijiji kutojihusisha
na shirikisho Hilo nchini.
Maamuzi hayo
yametolewa na uongozi wa shirikisho Hilo wakati wa uchaguzi wa viongozi
wa muda wa shirikisho Hilo kwa wilaya ya Iringa uliofanyika katika soko
la Mwamwindi Mlandege.
Akizungumza kwenye
mkutano huo, Katibu wa SHIUMA Taifa, Venatus Magayane alisema Kamati
Kuu ya SHIUMA iliyokutana hivi karibuni imejiridhisha pasipo shaka
kwamba Joseph Mwanakijiji anakosa sifa za kuendelea kuwa Naibu Katibu
Mkuu wa SHIUMA nchini na kutaka kutojihusisha na shirika Hilo nchini.
Alisema
akiwa Naibu Katibu Mkuu ,Mwanakijiji alishindwa kufanya kazi yake
ipasavyo na uongozi ulipofika hapa kuuliza kuhusu shiuma kwa wamachinga
walikuwa hawalitambui hivyo ameshindwa kuinadi SHIUMA na Katiba yake kwa
machinga wa Iringa pamoja na kwamba kwa kupitia shirikisho hilo
amekwenda mikoa mbalimbali nchini kulitangaza shirikisho hilo.
Aidha
Alisema kuwa chanzo kingine ni migogoro ya mara kwa mara ya wamachinga
wilaya ya Iringa ambapo baada ya kufuatilia migogoro na vurugu za mara
kwa mara zilizokuwa zikifanywa na machinga wa Iringa alisema wamebaini
kiongozi huyo alikuwa sehemu yake kinyume na katiba ya Shiuma.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanja aliwataka viongozi wa
muda wa Shiuma wilaya kuwaunganisha na kuwasajili machinga katika
shirikisho hilo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa viongozi wake.
Masanja
alitoa onyo kwa uongozi huo akisema atakayebainika kuhamasisha
vurugu,maandamano na migomo inayohatarisha amani na usalama wa mali na
raia wengine atachukuliwa hatua za kisheria na kutoa wito kwa jeshi la
Polisi kushughulika nao.
"Lengo
la shirikisho ni kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ya
wamachinga nchini hivyo yoyote atakayeanzisha migogoro isiyo na tija
atakuwa Hana nafasi kwenye shirikisho Hilo na ikitokea changamoto basi
Kuna umuhimu wa kukaa meza Moja kuliko kuanzisha migogoro isiyo na tija.
Alisema
kuwa SHIUMA ni chombo kinachofanya kazi na serikali katika kuwaendeleza
machinga na biashara zao. Jambo lolote linaloleta tofauti baina ya
pande hizo mbili litamalizwa kupitia meza ya majadiliano na sio kwa
kuhamasisha vurugu au maandamano ama maandamano.
Naye
mgeni rasmi Katika mkutano huo Katibu tawala wa wilaya ya Iringa
Michael Semindu alisema kuwa serikali imeahidi kuwapa ushirikiano mkubwa
wamachinga nchini wakati wowote
Alisema kuwa
Serikali Iko na wamachinga popote hapa nchini na kutoa ushirikiano na
kukaa kwenye meza ya mazungumzo kwenye changamoto yoyote inayojitokeza
Alisema
kuwa wilaya ya Iringa imeandaa idara ndogo ya serikali ambayo itafanya
kazi Kwa karibu machinga ya kufanya kazi pamoja kuondoa changamoto za
machinga zilizopo pindi zinapojitokeza.
Akizungumzia
ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyotoa
milioni 10 ya kujenga ofisi ya wamachanga alisema kuwa wanatarajia
kujenga ofisi ya kisasa na ya mfano ambayo itakuwa na kumbi ya mikutano
na ofisi mbalimbali ikiwemo ofisi ya afisa biashara kwa Lengo la kuiweka
pamoja na wamachinga kutatua kero zao.
No comments:
Post a Comment