September 09, 2023

SMZ kuendelea kuweka mazingira wezeshi sekta ya kilimo

Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inaendelea kukuza maendeleo ya kilimo kwa kuweka mazingira wezeshi, kuweka mikakati madhubuti ikiwemo kuweka fedha kwa ajili ya sekta ya kilimo ,utoaji wa pembejeo za uhakika ili kukuza sekta ya kilimo biashara.

Akifunga maonesho ya tano siku ya wakulima nane nane kizimbani waziri wa nchi afisi ya waziri mkuu sera bunge na uratibu Jenista Mhagama ambapo alisema hatua hiyo itaonesha kujali na kuthamini sekta ya kilimo na kuongeza tija na ustawi wa kiilimo kwa wa kulima .

Aidha alisema kuwa Nia ya serikali kupitia kilimo ni kuwapatia wakulima na wafugani unafuu wa mahitaji mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa Pembejeo nafuu kwa asilimia hamsini ya gharama zake .

Hata hivyo aliusia wanawake na vijana kuendelea kujikita katika sekta ya kilimo kwa kushirikiana na wizara ili kupata mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo.

Waziri wa kilimo, umwagiliaji, maliasili na mifugo m
Mh Shamata Shaame Khamis alifahamisha kuwa katika kufanikisha maonesho ya tano ya wakulima nanenane wizara  imezingatia maeneo muhimu kwa wakulima ikiwemo kutambua idadi sahihi ya vijana ili kupata fursa ya kushiriki,kutambua maeneo ya wakulima.


 Alieleza SMZ inampango mkakati wa kila wilaya pamoja na kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kufanikisha mapinduzi ya kilimo.

Katibu mkuu wizara ya kilimo umwagiliaji maliasili na mifugo seif shaaban mwinyi amesema matarajitio ya wizara ya  mara baada ya maonesho hayo ni kuleta jita ya kilimo biashara kwa wananchi hasa wanawake na vijana ili kuendelea kuongea pato la uchumi wa taifa nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Benki ya NMB, Nsolo Mlozi kwa upande wake alifahamisha kuwa katika kuendeleza dhamira ya serikali ya kukuza uchumi wa nchi kupitia kilimo biashara wameanzisha mfumo wa kutoa elimu kwa jamii, Elimu ya kifedha ili kuwawezesha wakulima na wafugaji kupata mitaji ya uhakika na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Washiriki wa maonesho hayo walisema uwepo wa jambo hilo kwenye nchi litaweza kuchochea wakulima na wafugaji kuzalisha bidhaa bora na za kiushindani.

Maonesho ya tano ya siku ya wakulima nane nane yamebeba ujuembe wa vijana na wanawake ni misingi imara ya mifumo endelevu ya chakula ambayo yalifunguliwa rasmi tarehe 1/8/2023na raisi wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dkt hussen ali mwinyi na kufikia kilele chake tarehe 10/8/2023 ambapo waziri wa nchi afisi ya waziri mkuu sera bunge na uratibu mh jenista mhagama huku akipata nafasi ya kutembelea mabanda mbalimbali katika maonesho na kupata fursa ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya maafisa wa kilimo wilaya .


No comments:

Post a Comment

Pages