September 15, 2023

UVCCM WILAYA YA KILOLO KUSAKA VIPAJI

 NA DENIS MLOWE,IRINGA


UMOJA wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, imeandaa mpango maalum wa kutafuta vipaji vya vijana kwa wilaya ya Kilolo unaotarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 22  mwaka huu.


Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti Uvccm wilaya ya Kilolo ,Injinia Aman Mdeka alisema mpango huo una Lengo la kuwasaidia vijana wa wilaya Kilolo kuibua vipaji vyao na kuviendeleza katika mtazamo wa kiajira zaidi huku akitanabaisha kauli mbiu ya ya mpango huo kuwa "Kipaji Changu Ajira Yangu".

Alisema kuwa Kuna changamoto kubwa kwa vijana katika kutambua kwamba vipaji vyao ni ajira tosha kwenye maisha hivyo njia pekee ni kuanza kuvitafuta ngazi zote za chini na kuwapa njia ambayo italeta ajira na mwisho kuongeza kipato Cha kijana na taifa kwa ujumla.

"Ifike wakati vijana watambue kwamba vipaji ni ajira tosha katika maisha hivyo sisi kama Uvccm tumeandaa mpango maalum wa kutafuta vipaji vya wilaya ya Kilolo na kuvifanya vitambue kwamba kipaji ni ajira kwao na tutafanya hivi kata kwa kata kuvipata" Alisema 

Injinia Mdeka alisema kwamba mpango huo wa utazinduliwa rasmi Katika mji wa Ilula ambapo utakuwa kata kwa kata kwa wilaya nzima ya Kilolo na kilele chake kitakuwa Novemba 24 mwaka huu kwenye siku ya vipaji duniani.

Alisema kuwa mpango huo wa kutafuta vipaji utahusisha Sanaa mbalimbali za michezo ya kuigiza, uimbaji, kucheza muziki (kudance), na vipaji vingine ambavyo vitajitokeza siku hiyo na kuwataka vijana wa wilaya ya Kilolo kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa tamasha Hilo. 

Alitoa wito kwa wadau mbali mbali kujitokeza kudhamini mpango huo ambao utakuwa endelevu kwa wilaya ya Kilolo na utawasaidia vijana kukuza talanta zao na mwisho kujiajiri kama ilivyo kwa wasanii wengine wakubwa nchini.

Aliongeza kuwa zawadi za mapango unatarajia kuwa kubwa na kusema kwamba siku ya uzinduzi vijana watajulishwa na kuongeza kuwa zawadi nyngn ni elimu kwa wale ambao watafanikiwa kushinda.

No comments:

Post a Comment

Pages