September 18, 2023

YAFUNGIA VITUO 3 VYA MAFUTA KWA MIEZI 6 KWA KUFICHA MAFUTA

 EWURA 


Na Magrethy Katengu


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji EWURA imevifungia Vituo 3 vya uuzaji mafuta kwa muda wa miezi 6 Camel Oil- Gairo Petrol Station chenye Leseni namba PRL 2019-164,PETCOM-Mbalizi Petrol.Station chenye Lessen namba PRL 2023-025,Rashal Petroleum Ltd - Mkalama chenye Leseni namba PRL 2019-034 huku vitatu vikiendelea kuchunguzwa kwa ajili ya hatua zaidi.



Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James  Andilile amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na changamoto ya  uhaba wa mafuta iliyotokea  mwezi Agosti na Septemba,2023 ambapo baadhi ya Wafanyabiashara wenye Vituo  kuficha mafuta kwa maslahi yao kusubiria bei kupanda hivyo wananchi kupata usumbufu wa kufanya shughuli zao za kiuchumi.


Hata hivyo amebainisha kuwa kutokana na ufichaji wa mafuta EWURA imevichukulia hatua Vituo 8 ambavyo vimejihusisha na tabia ya kuhodhi mafuta ambapo Septemba 4 ,2023  EWURA ilivifungia Vituo viwili vya CAMEL OIL MSAMVU MOROGORO na MATEMBA CHA TURIANI Leo hivyo vitatu na vitatu vitatu vipo katika uchunguzi kwa ajili ya hatua zaidi


"Kwa mujibu wa Sheria ya Petrol sura Na 392 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA ) imepewa jukumu la kudhibiti masuala ya mafuta pamoja na mambo mengine kuhakikisha kuna upatikanaji wa mafuta wakati wote na imepewa mamlaka ya kuwajibisha Vituo vinavyokiuka taratibu za leseni zao"amesema Dkt James


Mkurugenzi Mkuu amewasisitiza wafanyabiashara kutambua kuwa biashara ya mafuta siyo holela kwani Leseni zinazotolewa wajibu wa kutekeleza na EWURA inafuatilia utekelezaji wa Leseni zilizotolewa ikiwemo kwa wenye Maghala,Wamiliki wa Vituo,na wafanyabiashara wa Mafuta inapotokea masharti ya Leseni hayazingatiwi hatua lazima zichukuliwe


"Hata kama  tukimkuta mdau wa mafuta anafanya kinyume na taratibu za leseni yake kisheria anapewa notisi ya siku 21 ajitetee kwa maandishi na utetezi ukipokelewa wajibu wa EWURA ni kuchambua Utetezi pale endapo itajiridhisha pasipo shaka  hatua stahiki zitachukuliwa " amesema Dkt Andilile


 Aidha  onyo limetolewa  kwa Wafanyabiashara, wenye Vituo Maghala ya  Mafuta kutohodhi mafuta    kwani kumekuwa na tabia kila bei zinapoelekea kupanda wanapata jaribu la kuficha mafuta kusubiri bei mpya  hivyo bado vijana wanaendelea kuchunguza na atakayethibitika hatua kali za kisheria zitachukuliwa. 

No comments:

Post a Comment

Pages