Timu ya wakandarasi wa HUAWEI anaotarajiwa kutekeleza mradi huo akiwa tayari kwa kazi hiyo. |
Na Joachim Mushi, Dar
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohamed Khamis Abdulla leo amekagua vifaa vya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa mkongo wa taifa wa mawasiliano, awamu ya III sehemu ya ii, vilivyowasili tayari kwa utekelezaji wa zoezi hilo.
Akizungumza
katika tukio hilo, Bw. Khamis Abdulla amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mhandisi Peter R. Ulanga kuhakikisha mradi huo
unatekelezwa kwa wakati na katika thamani halisi kwa mujibu wa makubaliano.
Alisema
Serikali imeliamini Shirika la TTCL na kuliwezesha ili kuhakikisha linatekeleza
kikamilifu mradio huo, unaokwenda kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali
nchini Tanzania.
Kwa upande
wake, Mhandisi Ulanga alisema kwa kuweka umuhimu mradi huo, umeandaa Timu ya
Wasimamizi wa Miradi (Project Manager) ambao watakuwa na jukumu la kuhakikisha
wanasimamia miradi kikamilifu na kwa kuzingatia weledi.
“Tumewapatia
vitendea kazi ikiwemo magari kwa kila Msimamizi wa Mradi ili kurahisisha
shughuli katika kutekeleza miradi hiyo. Na bahati nzuri katika tukio hili leo
timu ya Wasimamizi wa Miradi wako hapa.
“Shirika la
Mawasiliano Tanzania tuko tayari kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya
Sita, ikiongonzwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania katika kuhakikisha miradi wa kuunganisha Wilaya zote nchi
nzima katika Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano inatekelezwa kikamilifu.
Akifafanua
zaidi alisema TTCL iko tayari kushirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari imefanikisha katika kukamilisha miradi yote ya
mawasiliano. Tunatambua dhamira ya Serikali katika kuwafikisha mawasiliano
Watanzania yenye ubora na yenye Uhakika,” alisema Mkurugenzi huyo.
Akitoa
ufafanuzi wa taarifa ya utekelezaji wa Upanuzi wa mradi huo wa Mkongo wa Taifa
wa Mawasiliano Awamu ya Tatu, Sehemu ya Pili alibainisha kuwa Upanuzi utafanyika
katika Wilaya 32.
“Upanuzi huu
unahusisha kufikisha Mkongo wa Taifa kwenye Wilaya 32, huku Wilaya 23 za mradi
huu ziko chini ya Mkandarasi wakati upanuzi kwenda Wilaya 9 unafanywa na
wataalamu wa ndani wa TTCL pamoja na upanuzi wa mzunguko wa Kaskazini na
Magharibi kutoka 800Gbps hadi 2 Tbps.
No comments:
Post a Comment