HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 05, 2023

KATWILA ASEMA UIMARA WA YANGA NDIO UMEWAPA MATOKEO

NA JOHN MARWA

BAADA ya Ihefu FC wana Mbogo Maji kuwachalaza Yanga SC Kocha wa Ihefu FC, Zuberi Katwila, amesema aliiangalia Yanga jinsi wanavyocheza na kuwaandaa wachezaji wake kuwa imara muda wote wa mchezo huo ulipigwa juzi na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.


Amesema kikubwa ni pointi tatu au moja, haikuwa mechi rahisi, walicheza kwa tahadhari kubwa na kuwaheshimu sana Yanga na kutumia makosa yao kupata alama walizozihitaji katika mchezo huo.


“Niliwapa tahadhari kubwa wachezaji wangu juu ya  ubora wa safu ya ushambuliaji ya Yanga kwani unaanzia  kwa viungo wao na tulifanikiwa kubana katika maeneo yao na kuzuia  njia zote za kupata ushindi nalo tulifanikiwa.


“Mabadiliko ya kikosi yameweza kunisaidia kwa sababu kuna wachezaji mechi iliyopita Saadun na Never Tigere walianzia benchi ikiwa (Super Sub) leo (juzi) nimewaanzisha ili kutafuta ushindi baadae niliwatoa na kuwaweka wengine na kuimarisha safu yangu ya ulinzi baada ya kuona washambuliaji wangu wamefanya kazi vizuri.” amesema kocha huyo.


Hata hivyo amewapongeza nyota wake kwa kuhakikisha wanafuata alichowaelekeza na kupata pointi tatu, kwa sababu haikuwa mechi rahisi kucheza na Yanga na kufanikiwa kupata ushindi na sasa wanaenda kutafuta pointi muhimu ugenini dhidi ya KMC FC. 

No comments:

Post a Comment

Pages