HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 04, 2023

NMB yapeleka tabasamu kwa Shule ya Awali na Msingi Uhuru, Sekondari ya Mawenzi na Anna Mkapa - Moshi

  

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru ya Mjini Moshi, ambao wamenufaika na msaada wa madawati 100 kutoka Benki ya NMB wakiwa na nyuso za tabasamu wakati wa hafla ya kupokea msaada  huo, pia NMB imetoa madawati na viti 50 kwa Shule ya Sekondari Mawenzi pamoja na Shule ya Sekondari Anna Mkapa. (Na Mpiga Picha Wetu).


Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mawenzi, Sella Sareyo, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati kwa shule za sekondari na msingi Moshi Mjini.

Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Uhuru, Lawrance Kissima, akisoma taarifa ya Shule ya Awali na Msingi ya Uhuru wakati wa hafla ya kupokea madawati 100 kutoka Benki ya NMB. Akitoa taarifa hiyo yenye wanafunzi 1128, Kissima amesema kuwa shule ilikuwa na upungufu wa madawati 172 lakini baada ya kupokea msaada wa Benki ya NMB shule hiyo sasa inaupungufu wa madawati 72 ambapo ameishukuru Benki ya NMB kwa kuboresha mazingira ya kujifunza na kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza ili kumaliza tatizo hilo. Aidha Kissima aliongeza kuwa shule hiyo kwa sasa inakamilisha mradi wa ujenzi madarasa manne na matundu matatu ya vyoo baada ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupeleka kiasi cha shilingi milioni 106.3 kupitia mradi wa BOOST.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Ladislaus Baraka, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 100 katika Shule ya Msingi Uhuru, pia NMB ilitoa madawati na viti 50 kwa shule za sekondari Mawenzi na Anna Mkapa vikiwa na thamani ya shilingi milioni 23.5 "Tunaipongeza Serikali kwa juhudi zake katika kusimamia na upatikanaji wa huduma bora za elimu mijini na vijijini. "Sisi kama wadau tunao wajibu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa kusaidia jamii zetu, kwani jamii hizi ndio zimeifanya benki ya NMB kuwa kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini". amesema Baraka.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori (kulia) akipokea sehemu ya msaada wa madawati na Viti 50 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Ladislaus Baraka (wa pili kushoto) kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mawenzi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, pia NMB imetoa madawati 100 kwa shule ya Awali na Msingi ya Uhuru. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Mawenzi, Sella Sareyo. 

 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori (kulia) akipokea sehemu ya msaada wa madawati na viti 50 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Ladislaus Baraka (wa pili kushoto) kwa ajili ya Shule ya Sekondari Anna Mkapa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, ambapo benki hiyo pia imetoa madawati 100 kwa Shule ya Msingi Uhuru. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Mawenzi, Sella Sareyo. 

No comments:

Post a Comment

Pages