Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu-Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Joseph Ngalawa (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 5 mmoja kati ya wanafunzi wanne waliofanya vizuri katika masomo ya Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Tatu Rajab Kikanda (wa pili kulia) katika hafla iliyofanyika chuoni hapo jana. Katikati ni Makamu Mkuu wa UDSM, Prof. William Anangisye na kushoto ni wazazi wa mwanafunzi huyo Hadija Sultani na Rajab Kikanda. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu-Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Joseph Ngalawa (wa pili kulia), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 5 mmoja kati ya wanafunzi wanne waliofanya vizuri katika masomo ya Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Esther Charles Maboja (wa pili kushoto), katika hafla iliyofanyika chuoni hapo jana. Kushoto ni Makamu Mkuu wa UDSM, Prof. William Anangisye na kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhasibu Shule Kuu ya Biashara UDSM, Dk. Patrick Mbwile. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu-Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Joseph Ngalawa (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 5 mmoja kati ya wanafunzi wanne waliofanya vizuri katika masomo ya Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Zubeda Hemed Bakar katika hafla iliyofanyika chuoni hapo jana. Kushoto ni Makamu Mkuu wa UDSM, Prof. William Anangisye. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu-Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Joseph Ngalawa (wa pili kulia), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 5 mmoja kati ya wanafunzi wanne waliofanya vizuri katika masomo ya Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rajab Fadhili Mchomvu (wa pili kushoto), katika hafla iliyofanyika chuoni hapo jana. Kushoto ni Makamu Mkuu wa UDSM, Prof. William Anangisye. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA MWANDISHI WETU
BENKI
ya NMB imewazawadia Wanafunzi Bora wa Mwaka wa Masomo ya Biashara wa
2022/23, waliohitimu katika Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM), ambako wanachuo wanne wamejizolea kiasi cha Shilingi
Milioni 20, sawa na Sh. Mil. 5 kila mmoja.
Hafla
ya kuwazawadia wanafunzi hao imefanyika UDSM, ambako Mkuu wa Kitengo
cha Rasirimali Watu – Huduma Shirikishi wa NMB, Joseph Ngalawa,
aliwakabidhi kila mmoja hundi ya mfano ya kiasi hicho, mbele ya Makamu
Mkuu wa Chuo, Profesa William Anangisye.
Tuzo
na zawadi hizo ni sehemu ya makubaliano yaliyosainiwa mwaka jana baina
ya NMB na UDSM, ambako taasisi hiyo ya fedha itakuwa ikiwazawadia
Wanafunzi Bora wa Degree ya Kwanza kwa Masomo ya Biashara wa chuo hicho
kwa miaka miwili mfululizo.
Kulingana
na makubaliano hayo ya mwisho wa mwaka jana, NMB ilipaswa kuwazawadia
wanafunzi watatu bora, lakini kutokana na wanachuo wawili kufungana
katika ufaulu wao, ikalazimika kuwatunukia wanafunzi wanne.
Wanafunzi
waliotwaa zawadi ya Sh. Milioni 5 kila mmoja na degree zao kwenye
mabano ni; Zubeda Hemed Bakar (Bachelor of Commerce in Banking and
Financial Services) na Rajab Fadhili Mchovu (Bachelor of Commerce in
Finance).
Wengine ni
Esther Charles Maboja na Tatu Rajabu Kikanda, ambao walifungana kwa
ubora wa ufaulu katika Bachelor of Commerce in Accounting, hivyo NMB
kuamua kuwatunukia wote na kufanya zawadi kufikia Sh. Mil. 20,
walizopewa wakishuhudiwa na wazazi na walezi wao.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Ngalawa alisema walisaini makubaliano hayo
kwa lengo la kuwapongeza wanachuo wanaofaulu vema katika masomo yao,
sambamba na kuchochea wanafunzi wengine waweze kufanya vizuri kwenye
masomo yao chuoni hapo.
“Tuko
hapa kuwapongeza na kuzawadia wanafunzi waliofaulu vizuri zaidi katika
mitihani yao ya kumaliza Degree ya Kwanza katika Chuo Kikuu cha UDSM,
tukiamini kuwa kufanya hivi kutawachochea wengine nao kusoma kwa bidi na
kupata ufaulu wao katika mwaka ujao.
“Huu
ni muendelezo wa ushiriki wetu katika ngazi mbalimbali za elimu nchini
Tanzania, ambako kwa Vyuo Vikuu tunazo program nyingi kwa ajili ya
wanafunzi, zikiwemo ‘Internship Program na Field Students Program.’
“Programu
hizo zinawapa uzoefu wanafunzi waliomaliza vyuo kuhimili ushindani wa
soko la ajira, lakini pia tunayo ‘Management Trainee Program’ kwa ya
wanafunzi wa Kitanzania wa vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi, kupata
mafunzo ya kuwa viongozi wa baadaye,” alisema Ngalawa.
Kwa
upande wake, Makamu Mkuu wa UDSM, Prof. Anangisye, aliishukuru NMB kwa
kukabidhi zawadi hizo kwa wanafunzi wake kama walivyokubaliana na kwamba
Sekta ya Elimu ya Juu inahitaji wadau wengi zaidi wa kuchagiza ufaulu
na ustawi wa elimu kama NMB.
“Wako
hapa kuwazawadia vijana wetu ikiwa ni sehemu ya makubaliano yetu ya
mwisho wa mwaka jana, kufanya hivi kunaongeza chachu na ari ya kujisomea
miongoni mwa wanafunzi, hivyo kuongeza ubora wa wahitimu wetu katika
soko la ajira,” alisema Prof. Anangisye.
Naye
Latifa Mbelwa ambaye ni Amidi wa Shule Kuu ya Biashara UDSM, alisema
ili kukidhi ya kutoa huduma tatu UDSM, chuo kinahitaji washirika mfano
wa NMB ili sio tu kuzawadia wanachuo bora, bali pia kukisaidia chuo
chake kujua program shindani kwenye ajira ndani na nje ya nchi.
“UDSM
tunatoa huduma tatu, za Utafiti ili kuleta mabadiliko chanya kwenye
jamii, kutoa huduma kwa jamii na kujenga uwezo kielimu kwa maana
kufundisha, ili kuzalisha wafanyakazi wanaoenda kuhudumu katika sekta za
umma na binafsi.
“Kwa
hiyo hili sio jukumu tu la chuo, bali na wadau wote ndio maana
tunawapongeza NMB kwa makubaliano tuliyoyasaini mwaka jana, ambayo
utekelezaji wake ndio huu,” alisisitiza Mbelwa, huku wanufaika wa zawadi
za NMB nao wakiishukuru benki kwa pesa walizopewa.
No comments:
Post a Comment